TIGO YAMZAWADIA MSHINDI WA KWANZA WA TIGO BEATS
Posted in
No comments
Tuesday, June 26, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
KAMPUNI ya Mawasialiano ya Simu za mkononi ya tigo
imemtangaza mshindi wa kwanza wa promosheni yao ya Tigo Beats.
na huyu ndiye mshindi wa Tigo Beatz |
"Siamini macho yangu" |
"Tunaendelea
kuhakikisha kuwa tunawapatia wateja wetu huduma na zawadi zinazoendana na thamani
ya fedha zao,” alisema Alice Maro na kuongeza
leo tunamtangaza mshindi wa kwanza |
“Simu za mkononi zimekuwa ni zaidi ya kupiga ama
kutuma ujumbe wa maandishi, sasa simu zinawawezesha watumiaji kucheza michezo
mbalimbali pamoja na kudownload nyimbo, huu ni ubunifu ambao tunaendelea
kuufanya ili kuhakikisha tunawapa wateja wetu kile wanachokitarajia kutoka
kwetu,” alisema Maro.
wakati wa kumtamshindi |
Kuhusu jinsi ya kushiriki katika promosheni ya Tigo
Beats, Maro alisema, kuwa kuna njia tatu za kushiriki ambazo ni, kubonyeza
alama ya nyota wakati wa kupiga simu, kutuma herufi ya wimbo wowote kwenda
15050 au kupiga 15050 na kununua wimbo unaoutaka.
Zumra na hundi yake ya sh. 10,000,000 |
Alibainisha kwamba mshindi wa promosheni hiyo
iliyoanza tarehe 26 Mei na kumalizika 19 julai mwaka huu, wateja watapata fursa
ya kujishindia Tsh. 5,000,000 pamoja na nyongeza ya Tsh. 5,000,000 kutoka Tigo na
hivyo kujinyakulia jumla ya Tsh. 10,000,000 taslimu.
Alice akimkabidhi Zumra Hundi yake |
Akiongea baada ya kupokea zawadi kutoka tigo, mshindi
wa Tsh. Milioni 10 za tigo beats, Zumra Mohamedi aliwataka watanzania kushiriki
katika promosheni hiyo bila kuchoka kwani mchezo huo ni kweli na wasikate tamaa
kama yeye alivyoshinda.
afisa uhusiano wa Tigo, Alice Maro akiongea na waandishi wa habari |
“nimefurahi sana yani siamini kabisa kama leo
nimeshika milioni 10 mkononi, niwaambie woteb wanaosema kwamba mchezo huu ni
danganya toto kwamba mchezo ni kweli na wajaribu kila mara bila kuchoka,”
alisema Zumra.
Zumra akiwa na baba yake mzazi |
Hata hivyo, alice alitoa tahadhari kwamba mshindi wa
promosheni atapatikana baada ya siku 60
kwa hiyo wateja wanatakiwa kushiriki mfululizo hadi mwisho wa promosheni
hiyo kama wanataka kuibuka washindi na kuongeza kwamba shindano la Tigo
linahusu kila mteja mradi tu awe ni mtanzania na awe na umri usiopungua miaka
18.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :