ALICHOKISEMA PREZZO KUHUSU KUPIGIWA KURA NA JAGUAR-BBA
Posted in
No comments
Saturday, August 11, 2012
By
danielmjema.blogspot.com

Prezzo akiongea na waandishi wa habari juzi baada ya kufika kwao Kenya akitokea Big Brother Africa South Africa.
Kama haufahamu ni kwamba Jaguar
ambae kwa muda mrefu wamekua wakirushiana maneno kwenye media na Prezzo
na kufanya watu waone wanabeef, aliweka tofauti zao pembeni na
kumsupport sana Prezzo wakati akiwa BBA kwa kupiga kampeni watu wampigie
kura ili ashinde.
Watu wengi walitamani kusikia Prezzo atasema nini kuhusu hiyo kampeni iliyofanywa na mtu ambae wanabeef (Jaguar).

Prezzo amesema “namshukuru
kama alinisimamia kwa kiwango hicho, ukienda kwenye show kama hii kwa
mfano unajua unakwenda kuwakilisha nchi yako so hata kama kuna uadui
wowote mnaweka kando kwa sababu nchi yako ndio inajalisha kwa hiyo mambo
mengine yote tunapuuzia mbali
Kwenye line nyingine President
CMB amesema “napenda kusema asante kwa kunipigia kura nashkuru, na u
know kama kawaida wakati wote tuko pamoja man binafsi unajua sina
uhasama na mtu yeyote yule u know, maisha ni mafupi unajua ukizidi
kununa unapunguza maisha yako ukizidi kucheka unaongeza maisha yako,
wakati wangu wa kucheka ndio huu na ntaendelea kucheka so ambao
wananiona nikicheka chekeni na mimi”

Kuhusu uwezekano wa yeye kupiga
kolabo na Jaguar baada ya kutangaza kwamba hana uhasama na mtu, CMB
amesema “hiyo daraja tutavuka tukifikia, kwa sasa hivi yani bado kuna
vitu vingi mi mwenyewe sijatulia hata vizuri, sijamaliza hata kutoa nguo
zangu kwenye mabegi so tukifika kwenye hiyo daraja tutaivuka then
wakati huo”
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :