CHADEMA wahutubia Morogoro mjini katika Oparesheni SANGARA
Posted in
No comments
Tuesday, August 28, 2012
By
danielmjema.blogspot.com

Katibu mkuu wa Chama chama cha Demokrasi na Maendeleo Dkt Wilbrord Slaa akiongoza umati uliohudhuria mkutano wa hadhara wa Operesheni
Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) baada ya mtu mmoja kudaiwa
kupigwa risasi na kufariki dunia wakati wengine wawili nao wakidaiwa
kujeruhiwa kwa kupigwa na risasi na askari wa jeshi la polisi.
Tukio
hilo lilitokea majira ya saa 5 asubuhi eneo la Msamvu barabara kuu Dar
es Salaam-Morogoro wakati askari hao wakiwatawanya umati mkubwa wa
wanachama na wafuasi wa chama hicho waliokuwa wakisubiri viongozi wa juu
wa chama hicho ili waandamane kuelekea katika mkutano wa hadhara
uwanja wa Ndege mkoani Morogoro leo.

Katibu mkuu wa Chama chama cha Demokrasi na Maendeleo Dkt Wilbrord Slaa akihutubia wananchi wa Manispaa ya Morogoro katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Ndege mkoani Morogoro.

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Morogoro waliojitokeza katika mkutano huo.

Mbunge wa viti MaalumChadema Suzan Mungi akimwaga sera za chama hicho.

Makamu Mwenyekiti Chadema Zanzibar Said Issa Mohamed akifafanua jambo kwa wananchi hao.

Aliyekuwa
mgombea ubunge jimbo la Igunda kupitia Chadema, Joseph Kashinde
akizungumza na wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.

Mbunge
wa jimbo la Ubungo Jijini Dar es Salaam John Mnyika akipanda jukwaani
wakati akiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege
Manispaa ya Morogoro.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :