UCHAGUZI KRFA KUFANYIKA SEPTEMBA 9
Posted in
No comments
Thursday, August 23, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Uchaguzi sasa kufanyika Septemba 9
USAILI
kuwania nafasi ya uongozi wa Chama cha Soka Mkoa wa Kilimanjaro
(KRFA), umefanyika mapema leo Agosti 22, chini ya Mwenyekiti wake Dr.
Haule na kushuhudia viongozi mbalimbali wakichaguliwa huku mdau wa
michezo na aliekuwa Mjumbe wa Villa Squad, Ally Kindoile, kupenya kwenye
usaili huo.
Katika
usaili huo ulioshuhudiwa na wadau mbalimbali wa michezo, ulifanyika
katika ofisi za Manispaa ya Moshi, ambapo nafasi ya Mwenyekiti
waliopita ni pamoja na Godluck Moshi na Charles Mchau, Makamu
Mwenyekiti Shaban Mwalimu na nafasi ya Katibu Mkuu msaidizi kwenda kwa
Ally Kindoile.
Aidha
nafasi zingine walizopita wadau hao wa soka wa Mkoa wa Kilimanjaro,
majina na nafasi zao kwenye mabano ni Kusianga Kiata (Mhani), Distin
Kilua na Abdala Husein (Wajumbe Mkutano Mkuu).
Wengine
ni Keneth Essau na Amri Kiula (Wawakilishi wa Vilabu), Denis Joseph
Msemo, Cuthbert Mushi na Nassor Muchi (Wajumbe Kamati ya utendaji) na
Salma Omari Mndaira (Mwakilishi TWFA).
Katika hatua hiyo, Uchaguzi wake unatarajia kufanyika Septemba 9,Ulili, Mkoani humo.
Hata
hivyo, Ali Kindoile alipozungumza na waandishi wa Habari, muda mfupi
baada ya usaili huo, alishukuru kwa kupita kwake na kuhaidi kuendelea
kutoa ushirikiano katika kuinua soka la Mkoa huo, ambapo mipango yake
mbalimbali anatarajia kushirikiana na wagombea wenzake pindi
watakapofanikiwa kwa pamoja kupata nafasi hiyo hiyo Septemba 9.
“Tunaomba ushirikiano na umoja ili kufika mbali katika soka letu, umoja wetu ndio tutasaidia soka la mkoa huu” alisema Kindoile.
Kindoile
licha ya kuwa mdau wa michezo, aliwahi kuchezea timu mbalimbali
zikiwemo Simba B na Idrisa Fc, kwa sasa ni mdau mkubwa wa timu ya
Kilimanjaro Rangers ya mkoani humo na amekuwa mstari wa mbele katika
kusaidia vijana kwenye soka.
Uchaguzi huo awali ulitakiwa kufanyika Agosti 28, ambapo sasa umesogezwa mbele mpaka hapo Septemba 9.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :