Watu 48 Wauawa Kenya
Posted in
No comments
Thursday, August 23, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Polisi
nchini Kenya, wanasema kuwa watu 48, wameuawa kufuatia mapigano makali
kati ya jamii za Pokomo na Orma katika eneo la Mto Tana Kusini Mashariki
mwa Kenya.
Mauaji
hayo yilitokea wakati watu wenye silaha kutoka jamii ya Pokomo
waliposhambulia kijiji kimoja katika eneo la Reketa huku wakiteketeza
makaazi ya watu.
Naibu
kamanda wa polisi mjini Mombasa, Joseph Kitur, amethibitisha kuwa watu
48 waliuawa, 31 kati yao ni wanawake, watoto 11 na wanaume sita. Ng'ombe
wapatao 60 vile vile walikatakatwa na wavamizi hao.
Kitur
amesema shambulio hilo ni la kushangaza kwa kuwa watu 34 waliuawa kwa
kukatakatwa mapanga, wengine 14 nao waliteketea hadi kufa katika nyumba
zao.
Amesema uchunguzi wa awali umebainisha kuwa shambulio hilo lilifanywa na watu kutoka jamii ya Pokomo.
Tangu
mwezi uliopita, jamii hizo mbili zimekuwa zikipigana kuhusu umiliki wa
ardhi inayotumiwa kama eneo la malisho ya mifugo, lakini shambulio hilo
la Jumatano ndilo baya zaidi kuwahi kutokea katika historia yao. Ripoti
zinasema polisi wanawasaka wale waliofanya mashambulio hayo.
Kuna
taarifa kuwa watu kadhaa wamekamatwa na polisi lakini mkuu huyo wa
polisi hakuthibitisha ripoti hizo.Idara ya polisi imesema uhasama kati
ya jamii hizo mbili umekuwa ukitokota kwa muda, lakini hapakuwa na
ishara ya fununu yoyote kuwa shambulio hilo la Jumatano lingetokea.
Mwaka
wa 2001, takriban watu 130, waliuawa kwenye mapigano katika maeneo ya
mipakani kati ya jamii hizo mbili. Mbunge wa Eneo hilo, Danson
Mungatana, amesema shambulio hilo lilikuwa la kulipiza kisasi
mashambulio mengine yaliyofanywa na jamii ya Orma ambapo mamia ya mifugo
iliibwa.
Chanzo: http://www.bbc.co.uk/swahili/habari
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :