Dkt Bilal Afungua Mkutano Wa Walimu Afrika
Posted in
No comments
Monday, September 10, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa siku 3 kwa walimu wa nchi za Afrika unaojadili kuboresha Elimu kwa nchi za Afrika. Mkutano huo unahudhuriwa na wawakilishi wa walimu kutoka nchi saba za Afrika zinazotumia lugha ya Kiingereza katika ufundishaji. (Tarehe 10,Septemba 2012) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwaaga walimu kutoka nchi za Afrika wanaohudhuria mkutano wa 7 wa ACP, unaojadili kuhusu maboresho ya Elimu kwa nchi za Afrika. Mkutano huo umefunguliwa leo na Mheshimiwa Makamu wa Rais na unahudhuriwa na wawakilishi wa walimu kutoka nchi saba za Afrika hususani zile zinazotumia lugha ya Kiingereza katika ufundishaji. (Tarehe 10, Septemba 2012)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na wawakilishi wa walimu kutoka Kenya waliohudhuria
mkutano wa saba wa ACP unaojadili kuhusu kuboresha Elimu kwa nchi za
Afrika. Mkutano huo unahudhuriwa na wajumbe kutoka nchi saba za Afrika
mathalani zile zinazotumia lugha ya Kiingereza umefunguliwa leo na
Makamu wa Rais katika ukumbi wa Mlimani City Dar es salaam (Tarehe 10,
Septemba 2012).
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :