Z-Anto NA JAFFARAI NI MTU NA KAKA YAKE!
Posted in
No comments
Friday, September 7, 2012
By
danielmjema.blogspot.com

MSANII wa muziki wa kizazi kipya
bongo Z-anto kuwa hakuna kitu alichokuwa
anakijua kuhusiana na msanii
mwezake
Jaffarai lakini msiba uliotokea nyumbani kwao Mtwara ndiyo
uliowakutanisha na hadi wao kujuana kuwa wao ni ndugu wa damu , ambapo
Jaffarai ni kaka yake.
Msanii huyo aliichambua story
nzima hadi alipojua ishu hiyo kuwa Jaffarai ni kaka yake, kuwa kuna siku
moja alienda kusalimia nyumbani kwa Mtwara na alipofika huko, aliambiwa
kuwa Jaffarai katoka hapo kwao muda si mrefu, na baada ya hapo
alijiulizia maswali mengi kwamba jamaa alienda kwao kufanya nini.
Aliendelea kusema kuwa
hakuendelea kuhoji na baada ya siku mbili ulitokea msiba hukohuko kwao
na alipoenda kule alianza kutambulishwa na mama yake kuwa Jaffarai ni
kaka yake na hapo kwenye msiba kulikuwa na dada zake jamaa ambao nao ni
dada zake huku mama yake akimwambia walishindwa kuwaambia kwani ni
makosa ambayo tayari yalikwisha tokea.
“Utambulisho ule ulinifanya
niishiwe nguvu kwa sababu jamaa nilikuwa nashinda naye sana sehemu
sehemu na hata yeye hakuwahi kunaimbia ishu hii nahisi alikuwa hajui,
lakini hata hivyo nashukuru kwani sasa nimejua mshkaji ni kaka yangu na
nafurai sana,” alisema Z-Anto.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :