ZITTO KUGOMBEA URAIS 2015!
Posted in
No comments
Friday, September 28, 2012
By
danielmjema.blogspot.com

MHE. ZITTO ZUBERI KABWE, MBUNGE WA JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI KATIKA TIKETI CHA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MENDELEO (CHADEMA AMETANGAZA RASMI AZMA YAKE YA KUTAKA KUGOMBEA URAIS KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015.
AKIZUNGUMZA NA CLOUDZ FM, ALISEMA KUWA KATIKA UCHAGUZI HUO HATAGOMBEA TENA NAFASI YA UBUNGE KWANI ANADHANI KUWA KILE ALICHOKIFANYA KAMA MBUNGE KWA WATANZANIA NA WANAJIMBO LAKE LINATOSHA NA KWAMBA SASA AZMA YAKE NI KUWATUIMIKIA WATANZANIA NA WANAKIGOMA KATIKA NAFASI YA JUU YA UONGOZI.
ALISEMA KATIKA MUDA WAKE AMBAYO AMEHUDUMU KAMA MBUNGE AMEFANYA MENGI NA ANADHANI KWA SASA KILICHOMBELE YAKE KAMA MTETEZI WA WANYONGE NA SAUTI YA UMMA YA KITANZANIA NI KUIONGOZA NCHI HII KUFIKA KULE AMBAKO KILA MTANZANIA AMEKUWA AKITAMANI KUFIKA
"NIMEKUWA MBUNGE KWA MUDA MREFU NA NI MENGI TU NMEFANYA KAMA MBUNGE NA NAAMINI KATIKA HILO KILA MTU ANAJUA, SASA NI WAKATI WA KUTETEA MASLAHI YA WATU WANGU WATANZANIA NA KUWAONGOZA KWENDA KAANANI," ALISEMA ZITTO
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :