MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI MSIKITI MPYA WA JIHAD WILAYA YA MWANGA-KILIMANJARO

Posted in
No comments
Friday, October 26, 2012 By danielmjema.blogspot.com

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika Jengo la Msikiti mpya wa Jihad, baada ya kuzindua rasmi Msikiti huo uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro, leo Oktoba 26, 2012 wakati wa Sikukuu ya Eid El Hajj, iliyofanyika sambamba na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre. Picha na OMR
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini wa Dini ya Kiislam katika Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya wa Jihad, uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada hiyo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa Jiwe la Msingi pamoja na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre, leo Oktoba 26, 2012. Picha na OMR
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya wa Jihad, uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada hiyo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa Jiwe la Msingi pamoja na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre, leo Oktoba 26, 2012. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wananchi na waumini wa dini ya Kiislam, wakati akiondoka eneo hilo. 

Rais Kikwete ashiriki Swala ya IDDI kijijini Msoga

 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika swala ya Iddi katika Masjid Rajab kijijini kwake Msoga-Chalinze leo Asubuhi.
 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono wa Iddi na baadhi ya waumini walishiriki swala ya Iddi katika Masjid Rajab Kijijini kwake Msoga, kata ya Chalinze,Wilayani Bagamoyo leo asubuhi(picha na Freddy Maro)

RAIS DK SHEIN ASHIRIKI SALA YA EID EL HAJJ

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein,pamoja na Viongozi wengine
wakijumuika na waislamu na wananchi katika  swala ya EID el Hajj
katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
 
Baadhi ya Waislamu na wananchi wakisikiliza Hotuba,baada
ya Swala ya Eid el Hajj iliyotolewa na Sheikh Soraga,katika Msikiti wa
Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na waumini ya Dini ya
Kiislamu baada ya kuswali swala ya  EID el Hajj katika Msikiti wa
Mwembeshauri Mjini Zanzibar Leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .