PICHA NA MATUKIO MBALIMBALI ZIARA YA SIKU 4 YA JK. MKOANI KILIMANJARO

Posted in
No comments
Thursday, November 1, 2012 By danielmjema.blogspot.com

Rais Kikwete azindua kiwanda cha Kusindika Tangawizi Mamba Miamba

 Rais Jakaya Kikwete akiangalia chupa ya tangawizi iliyotayari kuuzwa mara baada ya Rais Kikwete kufungua rasmi kiwanda cha kuzalisha Tangawizi kimnachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mambakatika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi.
Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kinachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda wakati amkaribisha kufungua kiwanda cha kusindika Tangawizi.
 Rais Jakaya Kikwete akifungua rasmi kiwanda cha kusindika tangawizi katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi. Kushoto ni Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kimnachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda  na Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ambaye amefanikisha ujenzi wa kiwanda hicho kwa asilimia kubwa.
 Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ambaye amefanikisha ujenzi wa kiwanda hicho mara baada ya Rais Kikwete kufungua rasmi kiwanda hicho katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi. Kushoto ni Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kimnachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda
 Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kufungua rasmi langop kuu la Kiwanda hicho.
 Rais Jakaya Kikwete akikagua uzalishaji wa Tangawizi mara baada kufungua rasmi kiwanda cha kusindika Tangawizi kinacho milikiwa na Ushirika wa wakulima wa Tangawaizi katika Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi.
 Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kinachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda (kushoto) juu ya shughuli za uzalishaji mara baada ya Rais Kikwete kufungua rasmi kiwanda hicho katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ambaye amefanikisha ujenzi wa kiwanda hicho kwa asilimia kubwa.
 Rais Jakaya Kikwete akioneshwa chupa ya tangawizi iliyotayari kuuzwa .Kushoto  ni Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kinachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda akimpa maelezo  juu ya shughuli za uzalishaji mara baada ya Rais Kikwete kufungua rasmi kiwanda hicho katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi.
 Rais Kikwete akisalimina na wananchi wa rika mbalimbali waliofurika katika uiwanja wa michezo wa Goha kata ya Mamba Miamba kumsikiliza.
 Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi cheti cha shukrani Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela kwa kufanikisha ujenzi wa Kiwanda cha kusindika tangawizi katika Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro. Rais Kikwete alifungua kiwanda hicho juzi.
 Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecelaakizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kabla ya Rais Kikwete kuhutubia hadhara hiyo.
Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wakazi wa Kata ya mamba Miamba wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi.

RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI BARABARA YA MKUU ROMBO-TARAKEA na KUZINDUA UJENZI WA BARABARA YA KWA SADALA-MASAMA, WILAYANI HAI,LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaidiwa kuzindua jiwe la msingi na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na kupewa shukurani na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo.Kushoto ni Waziri wa Ujenzi,Mh. John Magufuli.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na washika dau wa miundombinu wakikata utepe  ishara ya kufungua rasmi  wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea leo Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaidiwa na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasini kukunjua pazia kama ishara ya kufungua rasmi  wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea leo Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne.Pichani kati akishuhudia tukia hilo ni Waziri wa Ujenzi Mh.John Magufuli.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasini kukunjua pazia kama ishara ya kufungua rasmi  wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea leo Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne.Pichani kati akishuhudia tukia hilo ni Waziri wa Ujenzi Mh.John Magufuli.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .