OBAMA ARUDI MAREKANI AKITOKEA DAR ES SALAAM
Posted in
No comments
Wednesday, July 3, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Rais Barack Obama wa Marekani leo
amekamilisha ziara yake barani Afrika.Ziara hiyo ameimalizia Tanzania alikowasili
hapo juzi ambapo jana asubuhi aliweka shada la maua katika eneo la mripuko wa
bomu kwenye ubalozi wa Marekani mjini Dar es Salaam.

Obama leo hii pia alitembelea mtambo wa umeme ulioko Ubungo mjini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kuwekeza dola bilioni saba kutanuwa mtandao wa huduma za umeme barani Afrika.
Jana usiku Obama alikuwa na mazungumzo na viongozi wa biashara.Tayari Rais huyo wa Marekani ameondoka nchini Tanzania . Awali ilizitembelea pia Senegal na Afrika Kusini.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :