Monday, May 9, 2016

POLE MDAU ISSA MUHIDDIN MICHUZI KWA KUFIWA NA MWANAO

Blogger na mpiga picha maarufu nchini, Issa Muhiddin Michuzi, anasikitika kutangaza kifo cha mwanae Maggid Muhidin kilichotokea jana Jumapili huko Durban, Afrika Kusini, alikokuwa masomoni.

Mipango ya kuusafirisha mwili wa marehemu inafanywa, msiba utakuwa Tabata Mawenzi jijini Dar es salaam ambako ratiba ya mazishi itatoka mara tu baada ya mwili kuwasili.

Habari ziwafikie ndugu, jamaa, majirani na marafiki popote pale walipo.

Innalillah wa inna ilayhi raajiun

No comments:

Post a Comment