CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Moshi kimedai kuwa Mwenyekiti wa
Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe amefilisika kisiasa na kumshauri kurejea
katika biashara zake.
Akizungumza
mbele ya wajumbe wa sekretarieti ya CCM ya Wilaya ya Moshi Mjini,
Katibu wa CCM wilayani humo, Aluu Segamba alisema Chadema inatafuta
kisingizio na kujenga chuki kwamba CCM itaiba kura mwaka 2015 jambo
ambalo alisema halijawahi kufanyika.
Kauli
ya CCM imetolewa siku chache baada ya Mbowe kutamka katika mikutano
yake mikoa ya Kusini kwamba iwapo CCM itasalimika mwaka 2015, atajiuzulu
siasa.
“Mbowe
alishashindwa siasa muda mrefu kwa hiyo asitafute kisingizio... ajue tu
mwaka 2015 CCM itashinda nafasi ya urais na wabunge likiwamo Jimbo la
Hai analoliongoza kwa sasa… huyu fani yake ni biashara aende huko,”
alisema Segamba.
Alisema
jambo wanalolalamikia Chadema kwa sasa la ugumu wa maisha ni la dunia
nzima na kutoa mfano kwamba bei ya sukari nchini ni Sh 2,100 wakati
Kenya ni Sh 3,000.
Aliongeza
kuwa hata mfumuko wa bei nchini ni asilimia 20 wakati Kenya ni asilimia
22 na kuhoji na huko nako kuna CCM? Segamba alikitaka chama hicho
kueleza wananchi hoja za msingi badala ya kuwadanganya na kuwajaza chuki
kwa masuala ambayo yapo wazi haswa kupaa kwa bei ya bidhaa kunakotokana
na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.
“Hoja
kwamba enzi za Mwalimu Julius Nyerere hakukuwa na matatizo siyo sahihi…
hawakumbuki wakati wa unga wa njano, sabuni na matatizo mengine lakini
hayo ni ya wakati huo, leo hii suala la mafuta ni la dunia Serikali
inafanya kazi nzuri na wananchi wanaona,” alisema.
Alitoa
mfano kuwa Serikali kwa sasa imewafikisha mahakamani viongozi
wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali zikiwamo za kupoteza mapato na
miongoni mwao wapo mawaziri, makatibu wakuu, wabunge na wakurugenzi wa
halmashauri za wilaya.
Katika
hatua nyingine, Katibu huyo alisema Chadema ambayo imeliongoza Jimbo la
Moshi mjini kwa miaka 15 haijajenga hata choo au barabara ya urefu wa
kilometa moja huku hali za maisha za wakazi hao zikiendelea kuwa duni.
Soma zaidi ...http://www.habarileo.co.tz

No comments:
Post a Comment