"Freemasons Ni Sawa Na Babu Wa Loliondo!"
Posted in
No comments
Thursday, June 14, 2012
By
danielmjema.blogspot.com

Ndugu zangu,
Jana jioni nilikaa na kusikiliza mazungumzo kwenye kijiwe cha kahawa cha kona ya Mtaa Swahili na Mkunguni pale Kariakoo. Mada kuu ilikuwa ni Freemasons. Nikashindwa kuvumilia kukaa kimya. Nikaonyesha kutaka kuchangia juu ya Freemasons. Kijiwe kikaa kimya kunisikiliza. Nikatamka; " Kwangu mimi Freemasons kwa Watanzania wengi ni dhana ya kufikirika kama ilivyokuwa kwa Babu Wa Loliondo. "
Kimya kikazidi kijiweni. Nikafafanua; Babu wa Loliondo , pamoja na kutangazwa sana, hajamtibu hata mgonjwa mmoja. Ni sisi Watanzania ndio ' wagonjwa' wa kuendekeza abrakadabra. Na Freemasons ni abrakadabra nyingine tunayolishwa Watanzania....
Ndugu zangu,
Mjadala ukawa mkali sana. Lakini, niliondoka pale Kariakoo nikiwa na hakika kuwa kuna niliowafumbua macho. Maana, ona ujinga huo kwenye gazeti la hapo pichani. Ukurasa mzima wa kwanza umepambwa na abrakadabra za Freemasons wakati leo ndio siku ya kutangazwa Bajeti, hakyamungu!
FADHILI
MOSHI.
0756 038 214
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako

0 MAOINI :