Msichana wa miaka 16 nchini
Kenya amefanya kituko baada ya kukosea na kupika bangi kama mboga kwa
ajili ya chakula cha familia jioni huko Kiarimui kwenye wilaya ya Embu..
Standard Media wamesema baba
mzazi wa huyo binti ambae ni mwalimu wa sekondari ana shamba nyumbani
ambalo lina mboga mbalimbali ambazo huwa zinanawiri wakati wote,
kiangazi na vuli.
Jioni hiyo mama wa huyo binti
alimuagiza mwanae ambae amerudi nyumbani kwa likizo kwenye kupika ugali
na mboga za majani, sasa mtoto alipokwenda shambani kuchukua mboga
hakuweza kutofautisha bangi na mchicha.
Sasa noma ikawa kwenye msosi
baada ya kuiva ambapo mtoto wa mwisho wa hiyo familia ambae ni wa kiume
alianza kucheka kucheka ovyo na ndio alikua wa kwanza wa kupakua msosi
mezani, alipomaliza kupeleka matonge mawili akasikia usingizi na
kuzimika hapohapo, wengine pia walipakua msosi na kweli na wao wakaanza
kucheka cheka ovyo.
Kingine cha ajabu wakati wako
mezani kuna mjusi alipita ukutani alafu wote wakaanza kucheka na kutoa
machozi baada ya kumuona, stori ilibadilika baada ya baba mwenye nyumba
kuanza kumfokea mkewe huku akisema anawapa watoto kazi ambazo sio saizi
yao.
Alipoinua mkono kumpiga mkewe
na yeye kicheko kikamzidi ambapo kwa mujibu wa huyo mpishi kisa kizima
kiliana kuwa kama movie na ikabidi waombe msaada kwa majirani ili
kuelewa kilichotokea.
Baadhi ya majirani walifikiri
kwamba huenda kuna majini yameipata hiyo familia ila wengine
wakasisitiza hao watu wapelekwe kwenye kituo cha afya ambapo baada ya
kupimwa damu zao zilikutwa zimejaa sumu ya dawa za kulevya, walitibiwa
na kurudi nyumbani ila baba mwenye nyumba anakabiliwa na mashitaka ya
kulima bangi shambani kwake.
Na mdau kutoka KENYA
No comments:
Post a Comment