IKIWA ndio siku ambayo chama cha madaktari nchini
kilitangaza kufanya mgomo wa nchi nzima, hali imekuwa tofauti katika hospitali
ya rufaa ya KCMC, iliyoko mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro kwa madaktari
kuendelea na shughuli zao kama kawaida.
Hii inakuja siku moja baada ya mahakama kuu kuamuru
madaktari kusitisha mgomo huo kufuatia serikali kutoa pingamizi kwa kuwepo kwa
mgomo katika mahakama hiyo hapo jana.
Madaktari hao walikutwa hospitalini hapo wakiendelea
na shughuli zao kama kawaida na hata walipoulizwa kuhusu mgomo, mmoja wa
madaktari wa hospitalini hapo, ambaye hata hivyo hakuwa tayari kujitambulisha
alisema wao wataendelea kutoa huduma kwa wagonjwa hadi pale watakapopata
taarifa rasmi kutoka kwa uongozi wa hospitali hiyo.
Juhudi za kuwapata viongozi wa hospitali hiyo
kuongelea hali hiyo zilishindikana baada ya kugoma kuzungumza kwa madai kwamba
wo sio wazungumzaji wa hospitali hiyo.
Wakiongea katika nyakati tofauti baadhi ya wagonjwa
truliofanya nao mahojiano katika wodi mbalimbali za hospitali hiyo, Aranyiaeli
Godson na Eva Kornel walikiri kupewa huduma kama kawaida.
“Hapa kwa kweli hatujashuhudia kitu hicho, wamekuja
kama kawaida na tunashukuru tumepewa dawa, tumechekiwa, kwa kweli hamna mgomo
hapa ila sijui labda kwa hapo baadae,”alisema Godson
Hata hivyo pamoja na kuwepo kwa huduma walisema
madaktari waliokuja kuwatembelea asubuhi ni wawili tu tofauti na ilivyo kawaida
ambapo huwa wanafika zaidi ya wanne kuwajulia hali.
“Ndiyo tunapewa
huduma madaktari tayari wamepita japo sio kawaida, leo wamekuj awawili tu
tofauti na kila siku huwa wanakuja hata wanne, watatu na siku nyingine hadi
watano,” alisema Eva.







No comments:
Post a Comment