MADEREVA MOSHI WAGOMEA USHURU WA MAEGESHO

Posted in
No comments
Wednesday, June 20, 2012 By danielmjema.blogspot.com


MADEREVA wa daladala za mjini moshi zimegoma kuingiza magari yao barabarani kwa madai kwamba ushuru wanaotozwa kama malipo ya stika za manispaa pamoja na ushuru ya maegesho kuwa ni kubwa mno.
Madereva hao walifikia uamuzi huo ikiwa ni wiki moja baada ya wenzao wanaofanya usafiri katika barabara ya pasua kugoma kupakia abiria kwa malalamiko kama hayo lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa maslahi yao na malalamiko yao yanasikilizwa na kufanyiwa kazi.

Wakiongea na gazeti hili mapema leo madereva hao walisema kuwa wamelazimika kugoma ili kuishinikiza halmashauri ya manispaa ya moshi kuangalia upya ushuru wanazozitoza ambapo katika tangazo lililotolewa na manispaa hiyo lilionesha ongezeko la ushuru kuanzia tarehe 1 julai mwaka huu.

Walisema ongezeko hilo ambalo linaonesha kuwa kila gari litatakiwa kulipa ushuru wa shilingi 1500 kutoka katika ule wa sasa wa shilingi 1000 pamoja na malipo ya stika ya manispaa ya shilingi 10,000 kwa mwaka ni uonevu kwani ushuru huo ni mkubwa sana na haiendani kabisa hali halisi ya maisha.

Katika ongezeko hilo pia wapo madereva wa teksi ambao watatakiwea kulipa ushuru wa shilingi 500 kutoka katika shilingi 200 wanayolipa sasa na madereva wa magari makubwa ambao watalazimika kulipa ushuru wa shilingi 2000.

Akizungumza  baada ya kukutana na uongozi wa manispaa ya moshi chini ya mheshimiwa mstahiki meya wa moshi, mwenyekiti wa usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro, Christopher Lyimo, alisema kimsingi wamekubaliana na mstahiki meya kusitisha mgomo hadi tarehe 25 mwezi huu huku akianisha maklubaliano yaliofikiwa na pande zote mbili kuwa ni pamoja na kusitisha utekelezaji wa ushuru mpya uliotangazwa.

Makubaliano mengine yaliofikiwa ni kusitisha mgomo huo, kufuta malipo ya stika, na kuongeza kiujumla kuna malalamiko mengine 11 ambayo manispaa imeafiki kuyafanyia kazi na kusisitiza kwamba kama mkutano wa tarehe 25 hautatoa ufumbuzi wa malamiko ya basi hawatakuwa na budi zaidi ya kuendelea na mgomo wao.

“tumekubaliana kusitisha mgomo, kufuta ushuru huu ambao hatuelewi mantiki yake, tumekubaliana kwa pamoja kwamba malipo ya stika ya manispaa pia isitishwe, tutasitisha mgomo hadi tarehe 25, siku ambayo tutakutana tena na manispaa isipokuwa kama maswali yetu hayatapatiwa ufumbuzi katika kikao hicho basi mgomo utakuwa palepale”, alisema Lyimo.

Kwa upande wake mkuu wa usalama wa barabarani mkoa wa Kilimanjaro, SSP- Peter N. Sima, aliyeongea kwa niaba ya mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro, alisema wao kama polisi hawatakuwa tayari kuvumilia vitendo viovu vya uvunjifu wa amani na kuwataka wananchi kutopenda kufanya vurugu inapotokea tatizo.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .