MADIWANI wa chama cha mapinduzi CCM, wameema wao hawa husiki
katika kile kinachoendelea katika baraza la madiwani wa manispaa ya mjini moshi
kutokana na mtafaruku amba umekuwa ukifukuta katika baraza hilo katika siku za hivi karibuni.
Madiwani walisema kuwa katika baraza hili linaloundwa na
madiwani wengi wa CHADEMA, kumekuwa na mapungufu megi katika uongozi na
usimamiaji wa miradi ya maendeleo katika manispaa kitu ambacho kimekuwa
kikisababisha mkwaruzano wa mara kwa mara kati ya wananchi na uongozi wa manispaa.
Walisema katika vipindi ambavyo baraza limeongozwa na
Madfiwani wa CCM, hakujawahi kuwepo kwa malumbano kama
inavyojitokeza hivi sasa.
Akiongea katika mkutano wa hadhara wa CCM, uliofanyika
katika kata ya korongoni, katika manispaa ya moshi, katibu wa CCM wilaya ya
Moshi, Aloo Segamba alisema, mambo yanayoendelea kwa sasa katika baraza hilo ni thibitisho tosha
kwamba CHADEMA hawafai kupewa uongozi.
Segamba alisema, katika siku za hivi kumekuwa na mikwaruzano
mengi baina ya wananchi na uongozi wa manispaa na kutolea mfano tukio la hivi
karibuni la mgomo wa madereva wa daladala wakipinga kutozwa ushuru mkubwa wa
maegesho na manispaa hiyo.
“Kinachoendelea katika baraza hili linatosha kutupa picha
kamili ya aina ya uongozi ambao tungeuweka madarakani endapo tungeichagua
CHADEMA kuongoza nchi hii,” alisema Segamba.
Mwenyekiti wa wazazi CCM mkoa na mjumbue wa kamati ya siasa,
Thomas Ngawaiya, alisema kuwa kuichagua chadema kuongoza nchi hata kwa dakika
ni dhambi ambayo kama wananchi watadiriki
kuifanya katika uchaguzi wa 2015, matokeo yake yatakuja kuonekana katika kizazi
kinachokuja.
“Hawa watu ni mafisadi wakubwa kuliko hata ilivyo kwa CCM
wanayoinyoshea kidole kila kukicha, wanazunguka nchi nzima na viongozi wao wote
wakitumia jasho la mwananchi, jamani huu si ufisadi huu, alisema Ngawaiya na
kuongeza
“ tukifanya kosa la kuwapa nchi yetu watuongeza dhambi hiyo
itakuja kuonekana matokeo yake katika kizazi chetu cha baadae,” alisema
Ngawaiya.
No comments:
Post a Comment