MUAVI: "SENSA YA MAENDELEO TUJITOKEZE KUHESABIWA"

Posted in
No comments
Monday, June 25, 2012 By danielmjema.blogspot.com

IKIWA zimesalia chini ya mwezi mmoja tu kabla ya sense ya mwaka huu kufanyika, jamii imeaswa kushiriki kikamilifu katika tukio hilo la kihistoria nchini kwani ndio njia pekee ya kuirahisishia serikali kazi ya kupanga mipango ya maendeleo.

Kauli hiyo ilitolewa na mratibu wa sense mkoani Kilimanjaro Alex Muavi akiongea na KIJIWEBLOG mara baada ya kuhudhuria kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa, RCC iliyofanyika hivi karibuni katika ofisi ya mkuu wa mkoa wakati akizungumzia maandalizi ya timu ya sensa katika kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanikiwa kama ilivyopangwa.

Muavi alisema timu ya sense hasa mkoani hapo iko tayari kuhakikisha kila raia anapata haki yake ya msingi ya kuhesabiwa na kuingizwa kwenye orodha ya serikali.

“Timu yangu haina mashaka kabisa , tumejiandaa, kila kitu kikosawa ili kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata fursa ya kuhesabiwa na kuingia kwenye daftari la kumbukumbu,” alisema Muavi.

 Alisema shughuli itaenda kama ilivyopangwa na kuongeza kuwa kwa mwaka huu wamejipanga kuhakikisha makosa yaliojitokeza katika sensa ya awali hayajitokezi tena.

“Tutahakikisha tunatenda haki katika kwa kila mtu na nadhani kama mambo yatakwenda kama tulivyopanga, basi yale mapungufu yote yaliyojitokeza katika sensa ya mwaka 2000 hayatajitokeza tena,” alifafanua Muavi.

Alitoa wito kwa watanzania wote hasa jamii ya wafugaji wa kuhamahama, wafanyabiashara na wafanyakazi kuwepo majumbani siku ya tukio, ili kutoa nafasi kwa timu ya sensa kufanikisha kazi yake.

“Ndugu zangu wafugaji wa kuhamahama, wafanyabiashara na wafanyakazi wengine kama mimi ni vyema tukatenga muda wetui na kutulia majumbani ili kushiriki katika zoezi hili la kihistoria,” alisem,a Muavi. 

Sensa ya mwaka huu ambayo kauli mbiu yake ni “sensa ya maendeleo jiandae kuhesabiwa” ni sensa ya 5 kufanyika tangu uhuru na inafanyika takribani miaka 12 tangu ilipofanyika kwa mara ya mwisho mwaka 2000.

MWISHO.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .