OPERESHENI ZUIA UHALIFU YANASA MBAO 79 MOSHI
Posted in
No comments
Thursday, June 21, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
JESHI la polisi mkoani kilimanjaro linamshikilia mtuhumiwa
mmoja mkazi wa kibosh manushi, manispaa ya moshi vijijini, wilayani kilimanjaro
kwa kosa la kuvuna miti bila kibali.
Akitoa ripoti ya mafanikio ya operaesheni kuzuia uhalifu
mkoani hapo mkuu wa jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro, kamanda Robert Boaz,
alisema jeshi hilo kupitia kwa operesheni hiyo ijulikanayo kama operesheni zuia
uhalifu, ulifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na mbao 79.
Alisema kwamba jeshi hilo lilipata taarifa kutoka kwa raia
wema na mara moja kufika nyumbni kwa mtuhumiwa huyo aliyemtaja kuwa ni Beda
Mallya Mmasi, akiwa nyumbni na walipombana aliwaonesha alipoku amezihifadhi
mbao.
Boaz alisema, kuwa hadi sasa hawajafanikiwa kujua thamani
kamili ya mbao hizo pamoja na aina lakini wanafanya mawasiliano na iodara ya
maliasili ili kuweza kujua thamani na aina ya mbao zilizokamatwa.
Operesheni zuia uhalifu mkoani Kilimanjaro ilianzishwa
tarehe 8 juni mwaka huu na tayari kwa msaada wa wananchi imeshaweza
kukamata watuhumiwa 25 wakiwa na 28.5kg
za mirungi, 83.5 kg za bhangi ambapo jumla ya watuhumiwa 14 walikamatwa.
Alisema kuwa tayari jeshi limekamata jumla ya watuhumiwa 14
wakiwa na lita 105 za pombe haramu aina ya gongo, watuhumiwa 2 wa unyan’ganyi
wa kutumia silaha pamoja na katoni 62 pombe bandia ya konyagi aina ya viroba zenye
viroba 144 ambapo watu 3 walikamatwa wakiwa na mitambo 2 ya kutengeneza pombe
haramu ya moshi.
Aidha kwa upande wa makosa ya usalama barabarani, kamanda boaz
alisema, jumla ya madereva 376 walikamatwa na makosa 711 ambapo katika makosa
hayo tayari tozo la ‘notification’ lililolipiwa Tsh. 23,630,000.
Makosa hayo ni pamoja na mwendo kasi wa magari, ubovu wa
magari, madereva kutokuwa na leseni, magari kutokuwa na leseni, kuzidisha
abiria na magari kutokuwa na bima.
Mdau wetu, Moshi.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako

0 MAOINI :