Sahihisho La Habari Kuhusu Jerry Muro

Posted in
No comments
Sunday, June 10, 2012 By danielmjema.blogspot.com


Jerry muro akiongea na waandishi wa habari

 Jana tuliweka hapa habari kuwa Jerry Muro anrudi TBC.Jerry mwenyewe ametupa ufafanuzi wa ziada ambao hatukuwa tumeupata kabla na kuwa hatakuwa mwajiriwa wa TBC bali atawauzia vipindi na atakuwa huru kuviuza TV yeyote.Hapa chini ni maelezo ya Jerry Muro.Tunaomba radhi sana kwa upungufu huo.
Msaidizi wa Mwenyekiti,Dar

UFAFANUZI WA JERRY MURO
Napenda kuwajulisha wanamabadiliko kuwa kuanzia jumapili tarehe 10 mwezi huu,saa tatu na nusu usiku nitaanza kurusha mfululizo wa vipindi vyangu TBC,lengo la vipindi hivi ni kuonyesha kazi mbalimbali zilizofanywa na serikali kwa kushirikiana na taasisi ya mkapa foundation haswa katika masuala ya afya.
Vipindi pia vitaonyesha changamoto mbalimbali tunazokabiliana nazo katika sekta ya afya ili kwa pamoja tuweze kuzitatua haswa katika maeneo ya pembezoni mwa nchi(vijijini).
Vipindi hivi nimefanya mwenyewe na kampuni binafsina vitarushwa TBC kwa ufadhili wa mkapa foundation.
Napenda ieleweke,mimi jerry muro sijaajiriwa TBC bali narusha vipindi vyangu pale kwa muda wa miezi miwili na nusu.
Mashabiki na wapenzi wa kazi zangu karibu tutazame ili pamoja tuweze kukabiliana na changamoto zinazolikumba taifa letu na hatimae tuweze kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania.
Naomba kuwasilisha,
Jerry muro.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .