TCRA WATOA SOMO KUHUSU MATAPELI MFUMO WA DIGITALI
Posted in
No comments
Saturday, June 23, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania, TCRA imewataka wananchi
kuwa makini na wafanyabiashara matapeli wanaouza vifaa na vyombo vya
mawasiliano wakati huu ambapo nchi inafanya mabadiliko katika mawasiliano
kutoka katika mfumo wa analogia kwenda mfumo wa digitali.
Kauli hiyo inakuja, kufuatia kuwepo kwa wimbi la
wafanyabiashara wanaowatapeli wananchi kwa kuwauzia televisheni zinazotumia
mfumo wa analogia kwa kuwadanganya kuwa mitambo hiyo ni ya kidigitali.
Angalizo hilo lilitolewa na mkurugenzi wa matangazo wa TCRA
na mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya kuelimisha umma kuhusiana na mabadiliko
ya mfumo wa mawasiliano, Habbi Gunze katika mkutano wa kamati hiyo na uongozi
wa mkoa wa Kilimanjaro.
“kumekuwa na wafanyabiashara matapeli ambao wamekuwa
wakiwalaghai wananchi kwa kuwauzia TV ambazo hazina uwezo wa kupokea
mawasilaino ya kidigitali kwa kubandika stika feki zikiopnesha kuwa vyombo
hivyo ni ya digitali kumbe sio,” alisema Gunze.
Kuhusu malalamiko ya bei za ving’amuzi, alisema kamati yao imekuwa mstari wa mbele
kuishawishi serikali kufuta kodi katika gharama za vin’gamuzi kitu ambacho
serikali imetekeleza kwa kufuta kodi hiyo katika bajeti yake ya 2012/13.
Awali akifungua mkutano huo, mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,
Leonidas Gama alisema, mpango wa kubadilisha teknolojia ya analojia inayotumika
kwa hivi sasa katika sekta ya utangazaji kwenda teknolojia mpya ya dijitali ni
mojawapo ya utekelezaji wa maazimio ya nchi zote wanachama wa umoja wa
mawasiliano duniani, ITU.
Gama alitoa wito kwa wananchi wote kuwa wepesi wa kupokea
mabadiliko kabla ya desemba 31 mwaka huu ambapo mitambo yote ya mawasilano
katika nchi za afrika mashariki zitapozimwa.
“tukubali tu kwa moyo mmoja kubadika kwa kununua vin’gamuzi
mapema, kubadilisha vyombo vyetu vya sasa, ili kuepuka usumbufu pale mitambo
yote ya mfumo huu wa sasa itakapozimwa,” alisema Gama.
Meneja wa TCRA, kanda ya kaskazini, Annete Mahimbo alisema,
kamati hiyo imekuwa ikizunguka nchi nzima kutoa elimu ambapo kwa sasa
wanatembelea maeneo ya miji mbalimbali na kuanzia kutokana na muda wanazunguka
katika kanda zote lengo likiwa ni kuwafikia watu wengi.
Alisema kazi yao
ni kuhakikisha wanakutana na wadau wote wa mawasiliano kabla ya desemba 31 ili
kuhakikisha elimu inawafikia watu wengi kwa haraka ili kuepuka usumbufu.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako


0 MAOINI :