Wanafunzi
wa shule ya Seminary Manow Wilayani Rungwe mkoani Mbeya usiku wa
kuamkia Juni 14 mwaka huu wamefanya uharibifu wa kuvunja mali ya shule
pamoja na kuiba vitu visivyo pungua dhamani ya shiringi milion 50.
Akiongea
na mwandishi mkuu wa shule hiyo ya Manow Watson Masiba amesema kuwa
mgomo huo ulianza mchana kwa kuwa wanafunzi hawakutaka kula Ugali bada
ya uongozi kuwaarifu kuwa siku hiyo hakutakuwa na ratiba ya wali kwa
kuwa mchele siku hiyo ulikuwa kidogo stoo,
Uongozi
wa shule ulipojitahidi kusuruhisha suala hilo kwa kaandaa chakula
hicho usiku huo lakini wanafunzi hao walianza kufanya vulugu kwa
kuvunja vioo vya majengo na kuvunja milango na kuiba kompyuta 11 za
shule pamoja na kuingia katika chumba cha kuandalia mitihani na kuchana
mitihani yote iliyo andaliwa kwa ajili ya kuanza kuifanya hapo kesho
tarehe 15.06.2012.
Kwa mujibu wa maelezo ya
wanafunzi na wana kijiji wanao izunguka shule hiyo imejionyesha kuwepo
kwa tofauti kati ya uongozi wa shule na wanafunzi hivyo kufikia
wanafunzi hao kutafuta sababu ya kufanya vulugu kwa kiasi cha uharibifu
wa mari za shule na kanisa.
Akiongea
na mwandishi Askofu Dr Esrael Mwakyolile amesema kuwa uharibifu ni
mkubwa sana na zaidi ya mali zisizo pungua shiringi milion 50
zimeharibiwa hivyo ameitaka serikali kupitia vyombo vya dola kuchukua
hatua kwa wale watakao bainika kuhusika na tukio hili kulipa fidia
pamoja na kuwa uongozi wa shule utawachukulia hatua za kinidham.
Naye
mkuu wa wilaya ya Rungwe Chrispin Meela kwa kushirikiana na kamati
yake ya ulinzi na usarama amekemea vikali kitendo kilicho fanywa na
wanafunzi hao ukizingatia shule hiyo ni ya Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri hivyo kuwa mfano wa tabia njema kuliko kuchukua hatua za
Kigaidi kuharibu majengo na kuiba mali za shule.
Amechumkua hatua ya kuifunga shule
hiyo hadi tarehe 02.07.2012 kwa kidato cha pili, tatu, Nne na sita kwa
kuwa imeonekana kuwa ndio viongozi wa uharibifu huo na wanafunzi
wajapo shuleni hapo waje na wazazi wao na maelezo binafsi kwa
barua.
Hadi mwandishi anaondoka hapo jeshi la polisi liliimarisha
ulinzi shuleni hapo na wanfunzi 24 wamefikishwa police kwa mahojiano
zaidi.
N mdau wa kijiweblog, Rungwe
|
No comments:
Post a Comment