Watanzania Watakiwa Kuhama Kutoka Analojia Kwenda Digital...
Posted in
No comments
Thursday, June 21, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Waanzania
wametakiwa kujiandaa kuhama katika mfumo wa mabadiliko ya Analojia
kwenda katika mfumo wa digital ambao hadi ifikapo Desemba 31 mwaka huu
matangazo ya anaelojia yatazimwa rasmi.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini hapa mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya
mawasiliano Tanzania (TCRA)Bw. Frederick Ntobi amesema kuwa kuanzia
januari 2013 wananchi hawataweza tena kutumia mfumo uliopo wa
sasa wa anaelojia.
Amesema
kuwa ili kwenda na utandawazi uliopo hadi ifikapo januari 2013 dunia
nzima itakuwa imehama katika mfumo wa kutumia anaelojia katika luninga
zao hivyo ni vema wananchi wakaanza kujipanga mapema ili kuhakikisha
kuwa kila mtu anafikiwa na huduma hiyo.
Ameongeza
kusema kuwa ili mfumo huo ukamilike ni vema jamii ikahakikisha kuwa
lazima inakuwa na kifaa kiitwacho kingamuzi ambacho ndicho kinatumika
katika kubadilisha mfumo ili kuweza kufanikiwa katika ubadilishaji huo.
Bwana
Ntobi ametaja faidsa ya kutumia mfumo huo kuwa ni pamoja kuwa na
matumizi bora ya masafa ,kupata huduma bora za ziada mfano kulipia bili
ya umeme,kutuma pesa pamoja na kupata intenet pindi uwapo kwenye
luininga zao,Pia alitaja faida ingine kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa
ajira kwa kuwa mfumo utachangia kuongezeka kwa makampuni mengi ya
utangazaji.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako

0 MAOINI :