Shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2012 lafanyika jana jijini Arusha, kundi la Contagious Crew lajinyakulia kitita cha sh. milioni moja

Posted in
No comments
Sunday, July 1, 2012 By danielmjema.blogspot.com


Mmoja wa majaji wa shindano la  Serengeti Dance la Fiesta 2012 lililofanyika kwenye Club ya Mawingu jioni ya leo,jijini Arusha ,Hamis Mandi a.k.a B Dozen kutoka kipindi cha XXL kinachorushwa na redio ya Clouds FM,akikabidhi kitita cha shilingi milioni moja kwa kundi shindi la shindano hilo liitwalo Contagious Crew

Mwendesha shindano hilo pichani kati,Nikson akisoma majina ya makundi mawili yaliyoingia fainali na hatimae kulipata kundi moja mahiri kabisa na kundi la Contigious Crew limeibuka mshindi na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni moja taslim na kreti moja ya bia ya Serengeti,ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Fiesta 2012.
Pichani majaji wa shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2012 wakijadiliana jambo wakati wa mchuano mkali wa shindano hilo lililokutanisha makundi manne,ambayo ni Tp Jackson,New Kings,B-Boy Dance pamoja na kundi la Contigious Crew.Kulia ni Jaji Msami kutoka THT na shoto ni Mtangazaji kutoka Clouds TV,Issa Kwisa

Sehemu ya washabiki wa Serengeti Dance la Fiesta 2012 wakivutiwa zaidi na shindano hilo lilipokuwa likiendelea ukumbini humo.
Kila kundi lilionesha umahiri wake wa kucheza,huku kwa aliyeonekana kufanya vyema shangwe na miluzi ilitawala kila kona.
Palikuwa hapatoshi jioni ya leo ndani ya Club ya Mawingu wakati wa shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2012 likifanyika,ambapo kila kundi lilionesha umahiri wake wa kuyarudi mangoma kwa staili ya kipekee kabisa.Pichani mcheza shoo wa kundi la B-Boy Dance akionesha umahiri wake wa kucheza.
Vijana mbalimbali waliojitokeza kwa wingi kwenye shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2012,ambapo mshindi alifanikiwa kuibuka na kitita cha shilingi milioni moja na kreti moja la bia mshindi wa pili aliibuka na kreti la bia ya serengeti,ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo kwa mwaka huu.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .