Wanajeshi wa serikali iliyoangushwa Mali wateswa
Posted in
No comments
Wednesday, August 1, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binaadamu Amnesty
International limesema wanajeshi watiifu kwa serikali iliyoangushwa Mali
wameteswa na haki zao nyingine kukiukwa mikononi mwa jeshi lililofanya
mapinduzi.
Katika ripoti iliyotolewa leo nchini Ufaransa, shirika hilo limesema
wanajeshi hao aidha walitoweka au kuuawa mbali na kuteswa wakati
walipowekwa kizuizini baada ya kushiriki katika jaribio jingine la
tarehe 30 Aprili kutaka kulipindua jeshi lililokuwa limeiondoa serikali
ya kiraia mnamo Machi 22.
Mali Bamako Soldaten
Ripoti hiyo ya Amnesty International, ambayo inakuja siku kumi baada
ya ujumbe wa kutathmini hali halisi nchini Mali mnamo mwezi Julai, ina
matukio ya visa vya ukiukaji wa haki za binaadamu vilivyofanywa na
wanajeshi watiifu kwa uongozi wa kijeshi dhidi ya wanajeshi na polisi
waliohusishwa na mapinduzi ya pili ya kuliondoa jeshi.
Shirika hilo limewataka maafisa wa Mali kusitisha vitendo vya ukiukaji
wa haki za binaadamu na kuanzisha uchunguzi kuhusu visa kadhaa vya
kutoweka kwa watu, mauaji ya kiholela na mateso.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa
Hayo yanajiri wakati rais Traore akikabiliwa na muda wa mwisho leo
uliowekwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS
kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, ambayo inatarajiwa kuweza
kukabiliana na uvamizi wa upande wa kaskazini uliofanywa na wanamgambo
wa kiislamu wenye misimamo mikali.
Mara baada ya wakati mmoja kuwa nchi dhabiti kidemokrasia katika eneo
hilo, nchi hiyo ya Afrika Magharibi ilitumbukia katika mgogoro katika
nusu ya mwaka wakati waasi wa Tuareg walipofanya mapinduzi ambayo
yaliwakubalia wanamgambo kutwaa zaidi ya nusu ya nchi hiyo kwa upande wa
kaskazini.
Wangambo wametwaa udhibiti wa upande wa Kaskazini mwa Mali
Jeshi hilo likiongozwa na Kapteni Amadou Sanogo lilimwondoa
madarakani Amadou Toumani Toure mnamo tarehe 22 mwezi Machi, na
kukabidhi madaraka kwa serikali ya mpito ya kiraia, ambapo Rais wa mpito
Dioncounda Traore alichaguliwa kuiongoza mwezi Aprili.
Wanachama wa Amnesty waliwahoji watu 50 waliowekwa kizuizini katika
kituo rasmi, ambao awali walikuwa wakizuiwa katika mazingira mabaya
katika kambi ya kijeshi .
Wafungwa hao walisema walishuhudia watu 21 wakitoweka baada ya
kuondolewa katika vyumba vyao vya gereza katika usiku wa terehe 2 na 3
mwezi Mei.
Pia walieleza kuhusu mazingira ya kudhalilisha na hata vitendo vya
mateso na kuingiliwa kingono .Mfungwa mmoja alinukuliwa akisema katika
ripoti hiyo ya Amnesty kuwa mmoja wa wanajeshi aliingiza virungu
midomoni mwao, kuwazuwia kuongea.
Shirika hilo limezitaka Mahakama nchini Mali kuanzisha haraka uchunguzi
kuhusu madai haya na kurejesha utulivu katika nchi hiyo ambayo wananchi
wake wameathirika sana katika kipindi cha miezi sita iliyopita.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :