MKALI WETU
Posted in
No comments
Thursday, December 13, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Mwimbaji
wa Samboira anayetikisa anga za Bongo flev
Ben Pol, pichani
Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
KUNA nyimbo ambazo zinaweza kupigwa katika vituo vya redio
na televisheni bila hata kuchezesha kichwa, lakini si kwa wimbo wa
‘Samboira’. Wimbo huu uliombwa na msanii
mahiri wa muziki wa kizazi kipya, maarufu kama
Bongo Fleva, Ben Paul ‘Ben Pol’, unatamba katika vituo vya redio na televisheni
nchini.
Samboira una maana ya Jichinnge umeimbwa kwa lugha ya
Kinyambwa, yenye asili ya Tanzania,
inayounganisha makabila zaidi ya 120. Ben Pol, anatamba pia kwa sauti yake tamu
inayopita katika mioyo ya mashabiki wake kadhaa.
Kijana huyu, ametokea kupendwa kwa mashabiki weke wengi,
huku aina yake ya uimbaji ukiwa kivutio kwa watu wengi. Katika
mazungumzo na Handeni Kwetu, hivi karibuni, Ben Pol anasema kwamba
muziki ni kipaji chake.
Ben pol akiwa jukwaani
Anasema hali hiyo inadhihirisha katika aina ya utunzi wake,
uimbaji wake sambamba na manjonjo anayokuwa nayo katika kuhakikisha kuwa
mashabiki wake wanapata kitu adimu kutoka kwake na kufurahia kazi zake.
“Muziki ni kipaji changu nilichozaliwa nacho kutoka kwa
Mungu, huku nikiamini kuwa utanipatia maisha mazuri pamoja na heshimu kama wengine.
“Naamini katika hilo
nitafanya kila niwezelo katika kuandaa mashairi mazuri pamoja na nyimo ambazo
watu wengi watavutiwa nazo, ukizingatia kwamba muziki unahitaji umakini na
utundu wa hali ya juu,” alisema Ben Pol.
Mwaka jana Ben Pol aliingiza sokoni albamu yake ya kwanza
iliyokwenda kwa jina la ‘Maboma’ iliyokuwa na jumla ya nyimbo 10. Baadhi ya
nyimbo hizo ni pamoja na Maumivu, Maneno, Ninalinga, My Numbe 1 Fun, Samboira
na nyinginezo.
Ben Pol kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Pete aliyeimba
kwa hisia kali na kuburudisha mashabiki wake kutokana na uimbaji wake.
Msanii huyo aliyezaliwa jijini Dar es Salaam mwaka 1989,
anasema kwamba asili yake ni mkoani Dodoma, huku muziki wake akianza rasmi
mwaka 2009, aliposhiriki katika shindano la Nyuki Djs, akiwa na Linah Sanga.
Katika mashindano hayo aliweza kufanikiwa kutangaza kipaji
chake, hivyo kujiweka katiika mazingira mazuri, ambapo mwaka 2010, alikuwa
kwenye nafasi nzuri kuonyesha uwezo wake huku akiwa ni mwanafunzi wa kidato cha
sita, katika Shule ya Sekondari ya Azania.
Anasema hakuwa na usumbufu katika ufanyaji wake wa muziki,
maana wazazi wake wote walikuwa wanapenda yeye awe msanii, ingawa walitumia pia
muda wake kumpa ushauri wa kuendeleza zaidi elimu na muziki.
Anasema mwaka huo alifanikiwa kuachia wimbo wake wa kwanza
wa Shining Star, akirekodi katika Studio za Man Walter, jijini Dar es Salaam,
hivyo kumpa nafasi nzuri zaidi, hasa alipopata (label), mkataba wa ufanyaji
muziki katika Studio za M-Rabu.
Katika mkataba huo, alirekodi tena wimbo wake wa pili,
uliokwenda kwa jina la ‘Pata Raha’, katika kipindi cha mwaka mmoja tu, akiwa na
ndoto za kuwika katika anga za muziki wa kizazi kipya hapa nchini.
Ben Pol anasema kwamba malengo yake ni kufanya kazi nzuri
zaidi, ili kutangaza uwezo wake na kuwaziba midomo wasiopenda maendeleo yake.
“Muziki wangu nashukuru unapendwa na kila mtu, ndio maana
wimbo wangu mpya wa ‘Pete’ nao umepokelewa kwa shangwe na wadau wote hapa
nchini.
“Hata shoo zangu zinapendwa na watu wengi, hivyo naamini
nitazidi kushika nafasi za juu katika anga za muziki wa kizazi kipya pamoja na
kuchanua zaidi katika nchi mbalimbali duniani, ikiwamo Ulaya na kwingineko,”
alisema Pol.
Msanii huyo anasema kuwa hajapata tabu kutoka kwa wazazi
wake juu ya yeye kuingia kwenye muziki, maana walipenda mtoto wao afanye muziki
kwa ajili ya kutafuta maisha yao.
Pia anasema katika familia yao, akiwamo baba yake, alikuwa msanii ingawa
hajapata nafasi ya kufikia nafasi aliyokuwa nayo yeye. Hali hiyo inamfanya aone
kuna kila sababu ya kupiga hatua katika tasnia ya muziki wao nchini.
“Haya ni malengo yangu, nikiwa na hamu ya kuwa msanii nyota
pamoja na kutafuta nafasi ya kusoma zaidi elimu mbalimbali kadri nitakavyopata
nafasi.
“Nawaomba wazazi na wadau wote waendelee kuniunga mkono kwa
kuzipenda nyimbo na shoo zangu ili twende sambamba, maana sauti na kichwa
changu kinachangia kunifikisha hapa nilipo na kuongeza bidii zaidi,” alisema
Ben Pol.
Msanii huyo anasema kwamba muziki umekuwa na ushindani wa
aina yake, huku wasanii wenye kuumiza kichwa, wakizidi kupata nafasi ya kuwika
zaidi. Kijana huyo anasema kuwa anaamini ataendeleza mikakati yake ya kuwika
zaidi.
Ben Pol anasema kuwa ushindani wa muziki uliopo unatokana na
sanaa hiyo kuwaingizia kipati kikubwa wasanii wote nchini, hivyo kuonyesha kuwa
sanaa ni kazi.
Katika tamasha la Fiesta linalofanyika kila mwaka hapa
nchini, Ben Pol ni miongoni mwa wasanii waliofanya vizuri katika shoo hizo,
huku akikonga nyoyo za mashabiki wake katika baadhi ya mikoa aliyotembelea.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :