CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imewataka wananchi kusimamia Rasilimali zao kwa Kuwa ni wao ndio waathirika wakuu wa uharibifu na ufujaji wa Rasilimali unaofanyika sasa hivi.
Akizungumza na maelfu ya wananchi wafuasi wa chama hicho waliojitokeza kwa wingi katika mikutano hiyo, Katibu Mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Dkt. Wilbroad Slaa alisema kuwa ncwaandamizi wa chama hicho, itaka serikali kutoa ufafanuzi kwa wani hii inarasilimali nyingi, ukianza na mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama na madini ambayo kwabahati mbaya nchii imeshindwa kuzithamini kwa manufaa ya wananchi.
“Wananchi wa nchi hii, imefika muda ambao, tunatakiwa kutambua kuwa rasilimali zetu zinatakiwa zilindwe na Watanzania wenyewe, nchi hii ina madini mengi tu, tuna bahati ya kuwa na Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, madini ya uraniam, na vivutio vingi lakini kwa bahati mbaya rasilimali hizo tumeshindwa kuzifaidi na badala yake tumebaki kuwa masikini,” alisema.
Alisema kuwa endapo wananchi hawatazinduka na kupigania haki zao, swala la kuondokana na umasikini na uozo wa ufisadi ulitapakaa kila kona ya taifa hili haitafika mwisho zaidi ya kuendelea kutafuna mifuoa yetu hadi kaburini.
“Tunawashauri wananchi kujitambua na kupigana kwa pamoja kulinda rasilimali za nchi pamoja na kusukuma mbele lengo letu la kuleta ukombozi wa kifikra, ukombozi wa kimaendelea na ukombozi katika siasa ya nchi hii,” alisema dkt.Slaa
Dkt.
Slaa alisema ifikie muda sasa wananchi watambue kuwa vuguvugu la mabadiliko sio
jukumu la CHADEMA, bali ni wajibu wa kila Mtanzania anayejivunia taifa lake
huku akiweka wazi kuwa Chadema imeazimia kutumia mwaka 2013 kuwa mwaka wa nguvu
ya umma.
alisema kuwa katika moja ya maazimio ya CHADEMA kwa mwaka huu, wamelenga kuwaeleza wananchi ukweli kuhusu badhi ya maswala ambayo wao Kama CHADEMA wanafahamu ukweli huku serikali ikiendelea kuwafumba wananchi

Slaa alisema moja ya maeneo watakayoshughulikia ni swala la elimu huku akimtaka
Rais Kikwete kutoa ufafanuzi sababu za kushusha kiwango cha ufaulu kutoka
asilimia 100 hadi asilimia 70 na kuongeza kuwa kushusha kiwango cha ufaulu
kunasababisha taifa kuendelea kuzalisha wasomi mambumbu.
Kiongozi huyo pia alikemea tabia ya baadhi ya maofisa katika jeshi l apolisi kutumika katika siasa ambapo alisema kuwa serikali inachangia kwa kiasi kikubwa kuchafua Jeshi la polisi kwa kuwatumia kama mashushu katika mikutano ya CHADEMA.
Kauli
hiyo ilikuja baada ya ofisa mmoja wa jeshi la polisi, ambaye inadaiwa kuwa
amekuwa na tabia ya kukihujumu chama hicho katika wilaya ya same, kutokana na
tabia yake ya kuwazuia wananchi kushiriki shughuli za CHADEMA ambapo katika
kikao cha jana kilichofanyika katika uwanja wa Kwasakwasa, Same mjini ASkari
huyo, alikutwa akishusha bendera ya chama hicho muda mfupi kabla ya mkutano
kuanza.
Mbali
na hivyo pia askari huyo alionekana akichukua dondoo muhimu ya mkutano huo kitu
ambacho kidogo kisababishe kuwe na uvunjifu wa amani kutokana na wananchi
waliohudhuria mkutano huo kujaribu kumshambulia Askari huyo.
ihujumu
chamachasasNaye Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA), alisema
kuwa inawapasa vijana wote kufahamu kuwa ukombozi wa aina yoyote ile unahitaji
nguvu za vijana, unahitaji umoja na mshikamano bila kujali itikadi za siasa
wala dini.
“Vijana wa wenzagu, ukombozi sio lele mama, ukombozi na mabadiliko kiuchumi, kimaendeleo, mabadiliko ya elimu, mabadiliko na ukombozi yanahitaji ujasiri na uthubutu wa moyo kufanya maamuzi magumu,” alisema
Kuhusu swala la Gesi ya Mtwara, Heche alisema, utafiti unaonesha kuwa Gesi iliyopatikana Mtwara, ambao unaujazo wa Trilioni 35 na kuifanya Tanzania kuwa ya pili kwa uzalishaji duniani, inaweza kuwalisha Watanzania kwa zaidi ya miaka 200 bila kufanya kazi yoyote.
Alisema kuwa maandamano ya wananchi wa Mtwara ni matokeo ya serikali kuendesha mambo yake bila kuwashirikisha wananchi wake, hivyo kuitaka serikali iangalie namna ya kukaa meza moja na watu wa Mtwara na kuwaeleza watanufaika vipi kutokana na Gesi hiyo baada ya Gesi
kupelekwa Dar es salaam.

| Dkt.Slaa akiwasili mkoani kilimanjaro jana |
| Mbunge wa Arusha Mjini-Godbless Lema akifanya yake |
| Lema |
| Ni Mwendo wa M4C sasa |
Kwa
upande wake, Meya wa Moshi, Jafari Michael alisema kuwa CHADEMA kama chama
kinachosimamia mabadiliko hawatakuwa tayari kukaa kimya na kuona wafanya wadogo
wadogo (machinga), wananyanyasika lakini CHADEMA itawasimamia na kuwateta na ikibidi kuwapa elimu badala ya kuwafukuza na kuwabughudhi katika shughuli zao.
Aidha, Jafari alisema, ile dhana kuwa CHADEMA ni chama cha maandamano ni upotoshaji mkubwa na kuongeza kuwa maandamano ni haki ya mwananchi yeyote Yule anayejitambua na kuitaka serikali kujikita katika kutatua kero za wananchi wake na sio kutoa matamko yasiyo na msingi wowote.

No comments:
Post a Comment