LOWASSA MGENI RASMI SOKOINE MARATHON

Posted in
No comments
Saturday, March 30, 2013 By danielmjema.blogspot.com



WAZIRI Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika mbio za Sokoine Marathon, zinatakazofanyika, Aprili 12, mwaka  huu, wilayani Monduli, mkoani Arusha.


Lowassa
Mbio hizo zitafanyika katika kijiji alichozaliwa na kuzikwa waziri mkuu Edward Moringe Sokoine ikiwa ni siku ambayo taifa itaadhimisha kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo mkuu katika historia ya taifa la Tanzania.

Akithibitisha hilo Mratibu wa mbio za Sokoine Marathon 2013, Wilhelm Gidabuday aliiambia TAIFA LETU.com kuwa tayari wameshapata uthibitisha wa kuwepo kwa kiongozi huyo akiongozana na viongozi wengine wakuu wa nchi wakiwemo Mawaziri na Wabunge.

“Kutokana na wadhifa na heshima aliyokuwa nayo Marehemu Sokoine tumeona ni vizuri kuwaalika viongozi wetu wakuu wa nchi,n watu wengi tu watakuwepo, wabunge, mawaziri wakiongozwa na mheshimiwa Lowassa, wananchi wa kada  mbalimbali, lengo ni kumpa heshima inayostahili kingozi wetu,” alisema Gidabuday.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya maandalizi aliyepewa jukumu la kuwasiliana na viongozi ikiwa ni pamoja na Mgeni Rasmi, Mbunge wa viti maalum jimbo la monduli (CCM), Namelok Sokoine alisema kuwa, tayari wameshapata uhakika wa uwepo wa Lowassa katika mbio hizo.

Sokoine
likuwa tunatarajia kumpata kiongozi wetu wa nchi Mbio za Sokoine Marathon ambazo ni za kwanza kufanyika katika historia ya nchi hii katika maadhimisho ya kumbkumbu ya kifo cha kiongozi wa ngazi za juu wa taifa letu zinatarajiwa kushirikisha wakimbiaji zaidi ya 500 ambapo mpaka sasa tayari wanariadha 300 wameshathibitisha kushiriki.

Akizungumzia swala la kutoa namba pamoja na usajili, Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Arusha (ARAA), Joseph Jorwa alisema tayari utaratibu wa kuandaa namba umeshakamilika na kuongeza kuwa zoezi la usajili utafanyika baada ya sikuukuuu za Pasaka, katika Ofisi za ARAA, zilizoko katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kwa ada ya sh. 2000 za Tanzania.

Sokoine Marathon zitahusisha mbio za kilometa 10 na kilometa 2 kutembea na kukimbia na zitatanguliwa na misa maalum zitakazofanyika katika kanisa la katoliki alililokuwa ni muumini kijijini kwake na zinatarajia kukutanisha watu mbalimbali kumuombea kiongzi huyo.


Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .