Wednesday, March 6, 2013
MWENYEKITI WA JUKWA LA WAHARIRI NA MHARIRI MTENDAJI WA NEWHABARI (2006) INAYOCHAPISHA MAGAZETI YA MTANZANIA, AVAMIWA NA KUJERUHIWABSALOM KIBANDA AVAMIWA NA KUJERUHIWA
Mwenyekiti wa baraza la Wahariri Tanzania na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya NEWHABARI (2006)LTD, Ndugu Absalom Kibanda, amevamiwa na watu wasiofahamika usiku wa kuamkia leo akiwa anashuka Nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach, jijini Dar es salaam.
Taarifa zinasema kuwa Kibanda ambaye amepata majeraha makubwa kichwani hasa sehemu ya jicho amekimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kupata Matibabu.
Pole sana Ndugu yangu, bosi wangu Absalom Kibanda kwa Masahibu yaliyokukuta, hizi ni taarifa za kushtusha hasa katika tasnia hii ya Habari.
LAKINI SWALI LANGI NI KWAMBA MATUKIO KAMA HAYA MAANA YAKE NI NINI NA YATAISHA LINI....??



No comments:
Post a Comment