EU YAMWAGA NEEMA SAME-KILIMANJARO
Posted in
No comments
Sunday, May 19, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Shirika
la Misaada la Jumuiya ya Ulaya (EU) limetoa kiasi
cha shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya mradi wa uhifadhi endelevu wa
hifadhi ya mazingira ya asili ya Chombe, wilayani Same, Mkoa wa
Kilimanjaro.
Hayo yameelezwa na
mhifadhi mkuu wa wa hifadhi ya asili ya Chome, Frank Mahenge, wakati wa hafla ya kuutambulisha rasmi mradi huo, iliyofanyika
juzi, wilayani Same. Mahenge alisema kuwa
mradi huo utasaidia kuhifadhi mazingira ya Chome
ambayo yamekuwa yakiharibiwa na wananchi kutokana na kazi zisizo rasmi
wallizokuwa wakizifanya kwenye msitu huo wa asili ikiwa nipamoja na
kuchimba madini katika hifadhi hiyo.
“Hifadhi ya msitu wa
asili wa Come (SHENGENA) kulikuwa na zaidi ya
wachimbaji haramu 6,000 walikuwa wanaingia ndani ya hifadhi kwa siku
kwa madhumuni ya kufanya uharibifu ndani ya hifadhi hiyo, lakini
kutokana na juhudi kubwa za serikali pamoja na wadau mbalimbali
tumewatoa ndani ya hifadhi na kubaki wachache hasa wenyeji ”, alisema.
Hata hivyo Mahenge
alisema kuwa changamoto kubwa walizokuwa
wanakabiliwa nazo katika hifadhi hiyo ilikuwa ni ukosefu wa magari ya
doria,
ambapo ilikuwa ni vigumu kukabiliana na changamoto hizo, na ufinyu wa
bajeti na kwamba mradi huo mpya utakuwa chachu ya kuboresha mazingira
eneo hilo.
Aidha alisema mradi huo
ambao unatarajiwa kutekelezwa kwa muda wa
miaka miwili na nusu, utawashirikisha wananchi wa vijiji 27
vinavyozunguka hifadhi hiyo na unatarjia kuwanufaisha asilimia ya wakazi
wa vijiji hivyo ambao walikuwa wakiutegemea msitu huo na kusababisha
uharibifu mkubwa wa mazingira.
Mahenge alisema kuwa
shirika la misaada la jumuiya ya ulaya pia limetoa gari moja na pikipiki kwa ajili ya kuiwezesha hifadhi asilia ya chome kuweza kutekeleza majukumu yao.
Kwa upande wake, Mkuu wa
Wilaya ya Same, Herman Kapufi, alitoa wito kwa mamlaka husika katika
mradi huo
kuhakikisha fedha za mradi huo zinatumika kama ilivyo kusudiwa. Kwa
upande wake, Mkuu wa
Wilaya ya Same, Bw. Herman Kapufi, alitoa wito wka mamlaka husika katika
mradi huo kuhaklikisha fedha za mradi huo zinatumika kama ilivyo
kusudiwa.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :