NI CHELSEA VS BENFICA MOTO KUWAKA LEO; FAINALI EUROPA

Posted in
No comments
Wednesday, May 15, 2013 By danielmjema.blogspot.com

 http://cache.desktopnexus.com/thumbnails/1446071-bigthumbnail.jpg

DONDOO MUHIMU KUELEKEA MCHEZO WA LEO
 
Benfica wana Rekodi ya Mechi 31 kucheza na Klabu za England Barani Ulaya na Kushinda 10, Sare 5 na Kufungwa 16. Msimu huu, waliitoa Newcastle katika Robo Fainali ya EUROPA LIGI.

-Oscar Cardozo ameifungia Benfica Bao 6 katka Mechi 10 zilizopita dhidi ya Klabu za England.

-Chelsea wana Rekodi ya Mechi 8 dhidi ya Klabu za Ureno, 2 wakicheza na Benfica na 6 na FC Porto, na Wameshinda Mechi 6, Sare 1 na Kufungwa 1. Hadi sasa wamezifunga Klabu za Ureno katika Mechi 5 mfululizo na zote zikiwa ni kwa tofauti ya Bao 1 tu.

-Chelsea wanatinga Fainali hii wakiwa wameshinda Mechi 4 kati ya 5 kwenye Mashindano haya wakati Benfica wamefungwa Mechi 1 tu katika ya 11 walizocheza mwisho Barani Ulaya. 

Kipigo hicho kimoja ni pale walipofungwa 1-0 na Fenerbahce kwenye Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Mashindano haya na hicho ndicho kipigo pekee katika Mechi 38 tangu wafungwe 2-1 na FC Spartak Moskva kwenye UCL hapo Oktoba 23 Mwaka 2012.

Dondoo muhimu kwa Wachezaji:
 
-Oscar Cardozo wa Benfica ndie Mfungaji Bora wa 3 kwenye EUROPA LIGI Msimu huu akiwa na Bao 6, Goli 2 nyuma ya kinara Libor Kozak wa SS Lazio, na Fernando Torres anafuatia, pamoja na wengine wawili, akiwa na Bao 5.

- Čech, Oscar na Fernando Torres wa Chelsea na Kipa Artur wa Benfica ndio Wachezaji pekee waliocheza Mechi zote za Mashindano haya kwa Klabu zao.

-Aimar wa Benfica aliwahi kucheza chini ya Kocha wa Chelsea Rafael Benitez wakati wakiwa Valencia na kutwaa La Liga mara 2 na UEFA CUP Mwaka 2003/4.

-Beki wa Chelsea David Luiz alijitengenezea jina akiwa na Benfica Mwaka 2007 hadi 2011, akitwaa Ubingwa, kabla kuhamia Chelsea Januari 2011.

-Kiungo wa Chelsea, Ramires, aliisaidia Benfica kutwaa Ubingwa Mwaka 2009/10 kabla kuhamia Chelsea Agosti 2010.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .