DONDOO MUHIMU KUELEKEA MCHEZO WA LEO
Benfica
wana Rekodi ya Mechi 31 kucheza na Klabu za England Barani Ulaya na Kushinda
10, Sare 5 na Kufungwa 16. Msimu huu, waliitoa Newcastle katika Robo Fainali ya
EUROPA LIGI.
-Oscar
Cardozo ameifungia Benfica Bao 6 katka Mechi 10 zilizopita dhidi ya Klabu za
England.
-Chelsea
wana Rekodi ya Mechi 8 dhidi ya Klabu za Ureno, 2 wakicheza na Benfica na 6 na
FC Porto, na Wameshinda Mechi 6, Sare 1 na Kufungwa 1. Hadi sasa wamezifunga
Klabu za Ureno katika Mechi 5 mfululizo na zote zikiwa ni kwa tofauti ya Bao 1
tu.
-Chelsea
wanatinga Fainali hii wakiwa wameshinda Mechi 4 kati ya 5 kwenye Mashindano
haya wakati Benfica wamefungwa Mechi 1 tu katika ya 11 walizocheza mwisho
Barani Ulaya.
Kipigo hicho kimoja ni pale walipofungwa 1-0 na Fenerbahce kwenye
Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Mashindano haya na hicho ndicho kipigo pekee
katika Mechi 38 tangu wafungwe 2-1 na FC Spartak Moskva kwenye UCL hapo Oktoba
23 Mwaka 2012.
Dondoo
muhimu kwa Wachezaji:
-Oscar Cardozo wa Benfica ndie Mfungaji Bora wa 3 kwenye
EUROPA LIGI Msimu huu akiwa na Bao 6, Goli 2 nyuma ya kinara Libor Kozak wa SS
Lazio, na Fernando Torres anafuatia, pamoja na wengine wawili, akiwa na Bao 5.
- Čech, Oscar na Fernando Torres wa Chelsea na Kipa Artur wa
Benfica ndio Wachezaji pekee waliocheza Mechi zote za Mashindano haya kwa Klabu
zao.
-Aimar
wa Benfica aliwahi kucheza chini ya Kocha wa Chelsea Rafael Benitez wakati
wakiwa Valencia na kutwaa La Liga mara 2 na UEFA CUP Mwaka 2003/4.
-Beki
wa Chelsea David Luiz alijitengenezea jina akiwa na Benfica Mwaka 2007 hadi
2011, akitwaa Ubingwa, kabla kuhamia Chelsea Januari 2011.
-Kiungo
wa Chelsea, Ramires, aliisaidia Benfica kutwaa Ubingwa Mwaka 2009/10 kabla
kuhamia Chelsea Agosti 2010.
No comments:
Post a Comment