“Haukuwa uamuzi lahisi, lakini baada ya mjadala wa kutosha, tumeamua kujitoa mara moja kwa kuwa hata waandaaji (Cecafa) wameonekana kushindwa kuthibitisha usalama. Hivyo tunafanya hivyo kwa wachezaji wetu,” alisema Charles Obiny. Tusker imekuwa timu ya pili kujitoa baada ya Yanga ya Tanzania huku Simba na Falcon za Zanzibar nazo zikielezwa
AWALI....
YANGA YAJIVUA UBINGWA WA KOMBE LA KAGAME, CECAFA YAWAPA WAGANDA NAFASI YAKE
Mabingwa watetezi mara mbili wa
michuano ya Kombe la Kagame, Yanga wametangaza kujiondoa kushiriki michuano
hiyo.
Kupitia mtandao wake, Yanga
imethibitisha kujitoa katika michuano hiyo ambayo kama wangeshinda wangekuwa
wamebeba kombe mara ya tatu mfululizo.
Maana yake baada ya kushinda kombe hilo
mara mbili mfululizo, Yanga imeamua kujivua ubingwa.
Michuano hiyo imepangwa kufanyika
nchini Sudan na Yanga imechukua uamuzi huo kutokana na vigezo vya hofu ya
kutokuwa na amani ya kutosha nchini humo.
Hofu kubwa ilikuwa ni katika jimbo la
Darfur ambalo limekuwa na mapambano ya silaha mara kwa mara.

No comments:
Post a Comment