Rais wa Kwanza na Baba wa Taifa la Afrika Kusini, Nelson Madiba Mandela, kwa sasa yuko Hospitalini akipiganai Maisha Yake huko Pretoria Afrika Kusini. akiwa anatimiza Miaka 95 kesho Julai 18 mwaka huu, Mandela anabaki kuwa Mtu muhimu sana katika ukombozi wa Bara la Afrika kama sio nchi yake, Afrika Kusini.
Nelson Mandela ambaye watu wengi wanamchukulia kama kielelezo cha Uzalendo, anabaki kuwa mtu pekee ambaye Dunia nzima itaendelea kuenzi Uwepo wake hata kama atatuondoka leo au hata Kesho.
Swali la kujiuliza ni Je, Wangapi wanamfahamu Mandela? Wangapi wanafahamu kwa undani ni wapi alikotoka Shujaa huyu wa bara la Afrika? katika kuhakikisha hilo, TAIFA LETU.com imaendaa Makala Fupi ili kuwafahamisha Wapenzi wa Mzee huyu ni wapi alikjotoka na yey ni nani hasa.
Baba yake mzazi alifariki wakati Mandela akiwa na umri wa
miaka tisa. Kutoka wakati huo alilelewa na Jonintaba hadi wakati
alipoitoroka familia hiyo baada ya kutaka Mandela aoe katika ndoa ambayo
tayari ilikuwa imeshapangwa.
Wakati Nelson Mandela ‘Mzee Madiba’ alipoliongoza taifa la
Afrika ya Kusini dhidi ya ubaguzi wa rangi na kuibuka kuwa miongoni mwa
viongozi mashujaa duniani, tunapaswa kujuiliza ni watu gani katika
familia yake ambao walikuwa naye bega kwa bega wakimuunga mkono muda
wote.
Baba yake mzazi alifariki wakati Mandela akiwa na umri wa
miaka tisa. Kutoka wakati huo alilelewa na Jonintaba hadi wakati
alipoitoroka familia hiyo baada ya kutaka Mandela aoe katika ndoa ambayo
tayari ilikuwa imeshapangwa.
Tangu wakati Mandela alipoanza mapambano dhidi ya ubaguzi wa
rangi na kutafuta usawa kwa wote, ilitegemewa kuwa mke wake ndiye
angekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.
Mandela aliwahi kuwa na wake watatu katika historia ya maisha yake,
ambapo mke wa mwisho alimuoa siku alipokuwa akiadhimisha miaka 80 ya
kuzaliwa kwake.
Madiba anatajwa kuwa katika kipindi chote cha historia yake
amekuwa akiwaunga mkono watoto na upatikanaji wa elimu. Mfuko wa Nelson
Mandela wa kusaidia watoto ni sehemu tu ya ushahidi wa mafanikio ya
Mandela kuwasaidia watoto.
Mandela ni baba wa watoto sita. Watoto wanne aliwazaa na mke
wake wa kwanza, Evelyn Mase na watoto wawili aliwazaa na mke wake wa
pili, Winnie Madikizela.
Historia watoto wa Mandela
Wapo kati yao ambao hawakuwahi kwenda kumwona baba yao wakati akiwa gerezani.Watoto wake wote wawili wa kike aliowazaa na mke wa kwanza
walikuwa wakitumia jina la Makazawie. Mtoto wake wa kwanza alifariki
akiwa na umri wa miezi tisa na mtoto wa pili aliyejulikana kwa jina la
Madiba Thembikile (Thembi) alifariki katika ajali ya gari mwaka 1969
akiwa na umri wa miaka 25.
Mandela alikuwa gerezani na hakuruhusiwa
kwenda kuhudhuria mazishi ya mwanae.Mtoto mwingine, Makgatho alifariki kwa ugonjwa wa Ukimwi
mwaka 2005. Mandela amekuwa mstari wa mbele kupiga vita virus vya HIV na
Ukimwi akitumia namba 46664 ambayo ni namba yake alipokuwa gerezani
kupiga kampeni.
Mke wake wa Kwanza alikuwa ni Evelyne
Mandela na Evelyn walidumu katika ndoa yao kwa miaka 13 kabla
haijavunjika mwaka 1957. Evelyn alikuwa muumini wa dhehebu la Mashahidi
wa Yehova ambalo lilikuwa haliruhusu waumini wake kushiriki kwenye
siasa, hivyo muda wote hakujihusisha na siasa. Alifariki mwaka 2004.
Baada ya Evelyne alimuoa Winnie
Mandela alimwoa Winnie Madikizera mwaka 1958, ingawa muda
mwingi hawakuishi pamoja kwasababu Mandela alikuwa akitumikia kifungo
huku Winnie akijijengea umaarufu katika majukwaa ya siasa.
Alitalikiana na Winnie kabla ya Kumuoa Graca Machel
Kutokana na misuguano iliyoibuka ndani ya umaarufu wa kisiasa
ya Mandela na winnie walijikuta wakipeana talaka mwaka 1994. Mwaka
1998, Mandela alimwoa Graca Machel ambaye alikuwa mke wa kwanza wa Rais
wa Msumbiji, Samora Machel.

No comments:
Post a Comment