ABSALOM KIBANDA ATWAA TUZO YA DAUDI MWANGOSI;AANGUA KILIO UKUMBINI
Posted in
No comments
Thursday, November 7, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Mjane wa Daudi Mwangosi Itika Mwangosi kulia akifuatilia matukio yanayoendelea katika ukumbi huo |
WANAHABARI nchini
wametakiwa kujenga umoja katika
kupinga sheria kandamizi ya
vyombo vya habari na wanahabari
nchini inayatarajia kupitishwa na wabunge wa
bunge la jamhuri ya muungano wa
Tanzania.
Meneja wa uthibiti
wa ubora kutoka baraza la habari Tanzania (MCT) Pili
Mtambalike ametoa kauli hiyo leo
jijini Mwanza wakati wa
hafla ya
kukabidhi tuzo ya kishujaa na uandishi uliotukuka
ya Daudi Mwangosi .
Mtambalike amesema
kuwa idadi ya waandishi
kutekwa na kuuwawa imezidi kuongezeka
hapa nchini huku kasi ya
serikali kuvifungia vyombo vya habari
pia inaendelea kuongezeka .
Hivyo
iwapo wanahabari nchini hawataungana
katika kupinga manyanyaso
dhidi ya vyombo vya habari na kupinga
sheria kandamizi dhidi ya
vyombo vya habari na wanahabari
suala la uhuru wa
vyombo vya habari nchini litaendelea
kubaki ndoto.
Kwa upande wake rais wa umoja
wa vilabu vya
waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Keneth Simbaya alisema kuwa tuzo
hiyo inayotolewa ni tuzo ya
kwanza kutolewa nchini
Tanzania kwa waandishi wanaopata
matatizo wakati wanatekeleza
wajibu wao.
Simbaya alisema kuwa UTPC imeamua
kuanzisha tuzo hiyo kama
njia ya kuwapa moyo
wanahabari na kuuthibitishia umma
kuwa wanahabari nchini
hawatakata tama katika kutumikia
tasnia hiyo.
Alisema
iwapo jamii inapaswa kujua ni vema
serikali kukubali kutoa habari kwa jamii inayopasa kujua na
inayo haki ya kupata habari.
“
Serikali itambue kuwa inapohitaji
wananchi kuchangia maendeleo ni
vema itambue kuwa wananchi hao
wana haki ya kupata taarifa mbali mbali
ya kile walichochangia….ndani ya
tukio la mauwaji ya Mwangosi tumejifunza mambo mengi sana kwani
tunapofanya kazi zetu wapo
wasiopenda kuona tunafanya kazi zetu hiyo”
Pia alisema
ni vizuri wananchi kutambua kuwa wakati
wanahabari nchini wakitetea kupata
habari wasifikiri wanahabari wanajipangani
wao .
Kwani alisema
kuwa jitihada za wanahabari
kupigania uhuru wa kupata
habari zinapaswa kuungwa mkono na
kila raia wa Tanzania ambayo ana haki ya kupata
habari.
Jaji
mkuu tuzo hiyo Hamza Kasongo alisema kuwa mchakato
wa kumpata mshindi ulifanyika kwa kipindi cha miezi miwili kuanza septemba hadi Octoba
mwaka huu.
Tuzo hiyo ya
uandishi wa habari wa
kishujaa na utumishi
uliotukuka ya Daudi Mwangosi imetolewa kwa
Absalom Kibanda mahariri wa
kampuni ya new habari (2006) Ltd na mwenyekiti
wa jukwaa la wahariri nchini (TEF).
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :