MSAMA AZUNGUMZIA MAANDALIZI YA TAMASHA LA KRISMAS DESEMBA 25 MWAKA HUU

Posted in
No comments
Monday, November 11, 2013 By danielmjema.blogspot.com

3
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa tamasha la Krismas Bw. Alex Msama amezungumza na waandishi wa habari leo kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam na kuelezea maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika siku ya sikukuu ya Krismas kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushirikisha waimbaji mbalimbali wa injili kutoka ndani na nje ya Tanzania ametaja nchi ambazo washiriki watatoka kuwa ni Tanzania yenyewe, Afrika Kusini, Nigeria, Zambia, DRC Congo, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.

Ameongeza kuwa mmoja wa waimbaji hao kutoka Zambia natatarajia kuzindua albam yake mpya katika tamasha hilo. Msama pia amesema nusu ya fedha zitakazopatikana zinatarajia kulipia karo za shule kwa watoto wasiojiweza wapatao 300 na fedha nyingine zitaelekezwa kwenye ujenzi wa kituo cha misaada kwa w asiojiweza kitakachoitwa Jakaya Mrisho Kikwete Rafiki wa wasiojiweza kinachotarajiwa kujengwa huko Pugu, Kauli Mbiu ya Tamasha hilo ni 
 
"TANZANIA NI YA WATANZANIA TUILINDE NA KUIDUMISHA AMANI YETU"

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .