TAMKO LA WENYEVITI WA CCM-MIKOA LA KUMPONGEZA KATIBU MKUU WA CCM NDG. ABRAHAMANI KINANA NA SEKRETARIETI YA CCM TAIFA. LEO TAREHE 10/DESEMBA/2013 OFISI NDOGO YA CCM DAR- ES- SALAAM
Posted in
No comments
Tuesday, December 10, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Sisi
Wenyeviti wa CCM-Mikoa tuliokutana leo Tarehe 10/Desemba/2013 hapa Dar es
salaam, kwa kauli moja na kwa niaba ya wanaCCM wa mikoa yetu, tunatoa kauli ya
kumuunga mkono Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ndugu Abrahamani Kinana na
Sekretarieti yote kwa utekelezaji uliotukuka wa majukumu yao ya kichama. Tangu
alipopewa wadhifa wa Ukatibu Mkuu ameonyesha uwajibikaji mkubwa, uliokiwezesha
Chama kupata uhai mpya na kuamsha Ari na matumaini zaidi ya Watanzania kwa
Chama Cha Mapinduzi.
WanaCCM
nchini tuko katika mstari wa mbele kuisimamia Serikali yetu kwa mujibu wa Ilani
ya CCM ya mwaka 2010-2015 sura ya Tisa;
Inayokitaka Chama kuisimamia Serikali yake.
Kwa
pamoja tunaungana na kupinga kwa nguvu zote mambo yafuatayo;
1.
Ubadhirifu unaofanywa katika Serikali za Mitaa nchini unaozifanya
Halmashauri nyingi kujirudiarudia kupata hati chafu na zenye mashaka,
inayosababisha hasara na manung’uniko kwa wananchi.
2.
Utelezaji duni wa baadhi ya miradi ya maendeleo unaopelekea kuwepo
kwa huduma duni na zisizokidhi thamani ya fedha na matakwa ya kitaalamu. Hii
inaashiria uwepo wa Rushwa na ubadhirifu wa fedha kwa baadhi ya miradi ya
maendeleo.
3.
Ucheleweshaji wa maslahi na stahiki za watumishi wa Umma
kunakopelekea kuwa wavunja moyo na ari watumishi, katika kutekeleza majukumu
yao na hivyo kusababisha kutokea kwa migomo ya mara kwa mara kufuatia uzembe
katika kuwapatia haki zao, kinyume na misingi ya utawala bora.
4.
Gharama kubwa ya uendeshaji wa shughuli za Serikali na
Taasisi zake ikilinganishwa na gharama zinazotumika kwenye miradi ya maendeleo
na uboreshwaji wa huduma za jamii kwa wananchi.
5.
Usimamizi mbovu wa Operation mbali mbali za Serikali zenye
nia njema kwa Taifa. Mfano Operasheni kuhamisha wafugaji na Operasheni
Tokomeza; Zina nia njema lakini usimamizi wake umekuwa mbovu hata kupelekea
kuvuruga nia yake njema kwa Taifa.
6.
Kushindwa na Kuchelewa kutatua baadhi ya Kero sugu kwa
Wananchi kama malalmiko mbali mbali ya wakulima (mfano mbolea za minjingu
kutofanya vizuri kwa asilimia kubwa, matatizo ya wakulima wa pamba na korosho
nk.) na wafugaji; Rushwa zilizokithiri katika sehemu mbali mbali za utoaji wa
huduma kwa wananchi na ucheleweshwaji wa fadha za miradi ya maendeleo nk.
Katibu Mkuu wa CCM daima
amekuwa akikemea kwa nguvu zote madhaifu yote tuliyoyataja hapo juu na sisi kama
Wenyeviti wa CCM Mikoa yote Tanzania.
Tunaitaka Serikali ichukue hatua za haraka katika kurekebisha madhaifu hayo.
Viongozi na watendaji wengine wote wa Serikali, walioonesha udhaifu mkubwa
katika kutekeleza majukumu yao,
na ambao walipewa wito na wengine ambao wanatakiwa kupewa wito; wa kuhudhuria
mbele ya Kamati Kuu ya CCM wachukuliwe hatua zinazostahili. Tunawakumbusha
viongozi wa Serikali watambue kuwa Chama cha Mapinduzi kinaisimamia Serikali
kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya mwaka
2010-2015 Sura ya Tisa.
_______________________________________________
Mgana Izumbe Msindai –
Mwenyekiti wa Wenyeviti Mikoa
______________________________________________________
Haji Juma
Haji – Makamu Mwenyekiti Wa
Wenyeviti Mikoa
______________________________________________
Lucas Ole Mukusi –
Katibu wa Wenyeviti Mikoa
TUNAWASILISHA
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :