Mwanamke, je umeshawahi kushitukizwa mtoko (dating) na mwanaume wakati
wala ulikuwa huna mpango wa kutoka siku hiyo? Lakini pia umeshawahi
kujikuta ukiwa unamvutia kila mwanaume unayekutana naye pamoja na kwamba
hujajikwatua na urembo (Make Ups) kama ufanyavyo siku zote?





Ngoja niwamegee siri, Kuna baadhi ya vitu wanaume huvi-notice haraka
sana wamuanapo mwanamke zaidi ya muonekano wa wake wa kawaida. Vitu hivi
vinaweza kufunika maeneo ambayo hayakufanyiwa utanashati kwa siku hiyo,
kwa mfano mwanamke anaweza akawa hajatengeneza nywele zake kwa muda
mrefu au hajatengeneza kucha zale kwa muda mrefu, lakini inatokea pamoja
na udhaifu huo wanaume wakawa wanamkodolea macho kwa kuvutiwa naye
mpaka hata yeye mwenyewe akashangaa.
Ukweli ni kwamba pale mwanamke anapotoka salon au anapotumia muda mwingi
kujipamba akitoka anatarajia watu wamuone na waonyeshe kuvutiwa naye au
hata kuambiwa tu na watu anaokutana nao kwamba amependeza, wengi
hutarajia hivyo na ikitokea hakuna mwanaume anaye-notice kazi
aliyoifanya ya kujiremba hujiuliza maswali mengi sana na anaweza kurudi
kwenye kioo kujitazama upya ili kuona kama kuna mahali alipokosea.
Lakini pale ambapo hajajiremba yuko kawaida tu halafu ikatokea kila
mwanaume anayekutana naye anaonesha kuvutiwa naye na hata kuombwa mtoko
wa ghafla bila kutarajia, jambo hilo pia litamshangaza. Hapa chini
nitaeleza sababu.1. Usafi: haijalishi kama nywele zako ziko vululu vululu au nguo
uliyovaa sio nzuri sana na haifai kwa mtoko, usafi wa mwili kwa ujumla
huleta mvuto wa pekee. Mwanamke kuwa msafi bila kuweka vikorombwezo
vingine inatosha kumvutia mwanaume kiasi cha kuombwa mtoko. 2. Jifunze na shiriki michezo mbalimbali: Unaweza kuwa mcheza
mziki mzuri na mtu wa kujichanganya au unaweza kuwa mshabiki wa mpira wa
miguu na unazijua ligi mbalimbali au unaweza kuwa mcheza pool au Dats
mzuri, yaani jitahidi uwe mshiriki wa mchezo wowote utakaokukutanisha na
watu mbalimbali na kushiriki mijadala inayohusiana na michezo, jambo
hilo litakufanya uwavutie wanaume na kila mwanaume atamani kuwa karibu
na wewe au utakuwa unapata mialiko ya mtoko kutoka kwa wanaume
mbalimbali kwa sababu kuna kitu kinawavutia ukiwa nao karibu.3. Jiweke kisichana: Mavazi humbadilisha mtu kwa kiwango kikubwa,
kuna baadhi ya mavazi huwaweka wanawake kuwa kama watu wazima na kuna
mavazi huwapa muonekano wa kisichana. Kuna baadhi ya wanawake wana shida
ya kuchagua nguo za kuvaa, yaani hawajui ni nguo gani huwapendeza wao
wakiona mwanamke mwenzao kavaa nguo fulani na imempendeza na wao
wanakimbilia kununua na kuvaa bila kujua kama umbo lake linaendana na
nguo hiyo. Ni vyema wakati mwingie mwanamke akavaa nguo zinazomfanya
aonekane msichana zaidi na hivyo kwa na mvuto wa kipekee. Lakini ni
vyema zikiwa ni za heshima na zisiwe za kihuni zitakazokuvunjia heshima.
4. Kujitegemea: Je wewe ni aina ya mwanamke ambaye unasubiri
msichana wako wa kazi akusogezee kila kitu miguuni? Au wewe ni aina ya
mwanamke unayependa kutuma tuma na sio kufanya mwenywe? Kwa kawaida
wanaume hupenda wanawake wanaojitegemea, mwanamke ambaye hasubiri kila
kitu afanyiwe.
5. Kuwa na staha, subira na kuwavumilia wengine: Wanaume huwa
wana-notice kama mwanamke hana staha wala subira na ha wezi kuwavumilia
wengine. Mwanamke anaweza kuwa na mtoko na mwanaume lakini akifika
kwenye mghahawa anakuwa hana staka anapoongea na wahudumu lugha yake
inakuwa si ya kungwana na ni mwepesi kulaumu pale anapocheleweshewa
huduma. Hakuna mwanaume anayeweza kuomba mtoko na mwanamke wa aina hii.
Lakini mwanamke anapkuwa na staha, subira na wepesi wa kuwavumilia
wengine anakuwa na mvuto wa kipekee kwani lugha atakayokuwa anatumia
katika kuomba huduma itakuw ani ya kubembeleza na hata akichaleweshewa
huduma haonyeshi kisirani sana sana atauliza kwa upole huku akitabasamu.
6. Wepesi wa kusaidia:Kusaidia hapa haina maana ya vitu au fedha,
bali kuwatia moyo wengine, au kutoa msaada wa mawazo, ushauri nasaha au
kitu chochote kitakachomfanya mwingie ajisikie vizuri. Wanaume huwa
wanaangalia eneo hilo kwa makini, kama mwanamke ni mtu wa kujipenda yeye
zaidi yaani kila kitu anataka yeye awe wa kwanza na si mwepesi wa
kusaidia wengine inapoteza mvuto hata kama awe mzuri kiasi gani au
ajipambe kiasi gani. Mwanamke ambaye ni mwepesi kusaidia wengine na
anayependa wengine wajisikie vizuri wanapokuwa karibu naye anakuwa na
mvuto wa kipekee na kila mwanaume atavutiwa naye na kutaka kuwa naye
karibu7. Tabasamu: Jambo hili nimelizungumza sana, hakuna kitu
kinachomfanya mwanamke awe namvuto kama tabasamu. Mwanamke anaweza asiwe
mzuri wa sura na umbo au anaweza asiwe na mavazi mazuri wala mapambo ya
kuvutia, lakini tabasamu pekee linaweza kumpa nafasi ya kumvuto kwa
kila mtu atakayekutana naye.
8. Shiriki mazungumzo: Kama unatafuta mwanaume wa maisha yako,
basi shiriki mazungumzo, ni ajabu kwa baadhi ya wanawake wanaomba mtoko
lakini wanapokuwa kwenye mtoko wanakuwa wakimya na hawashiriki
mazungumzo, ni vyema kushiriki mazungumzo hata kama ni kupinga jambo
fanya hivyo kwa hekima na kwa kujiamini, yaani kuwa wewe, usiwe mtu wa
kuitikia tu kila mwanaume analosema, itakupotezea point. Wanaume
wanapenda kuwa na mwanamke anayesimamia kile anachokiamini na
anayeonekana kuwa na mwerevu.
9. Manukato: Hili halina mjadala, manukato kwa mwanamke ni muhimu lakini yasiwe makali sana kiasi cha kuwakera wengine.
10. Ukaribu na marafiki zako: Hakuna mwanaume ambaye anaweza
kuvutiwa na mwanamke asiyewathamini marafiki zake. Mwanamke ambaye
utafuiki wake na marafiki zake ni ule wa maji kupwa maji kujaa. Mwanamke
anaweza kuwa na marafiki wengi lakini si wote atakuwa na ukaribu nao
lakini inaweza kutokea akawa na angalau rafiki mmoja atakayekuwa na
ukaribu naye ambaye atakuw aakimshikikisha pale atakapohitaji ushauri
kuhusu jambo fulani linalomtatiza.
11. Kuwa mdadisi: Wanawake wengi wanadhani kwamba wanaume ndio wenye
jukumu la kuwashawishi ili wawapende, na hivyo hukaa kimya tu na
kusubiri wanaume waanze kujiongelesha na kujipigia debe. Wasichojua ni
kwamba hata wanaume wanapenda kuona wanawawake wakiwa na shauku ya
kutaka kujua mambo fulani fulani kuhusu yanayohusu maisha yao, hivyo
hutarajia kuona mwanamke akiwa mdadisi. Iwapo mwanamke atakuwa mdadisi
na kuonyesha kuvutiwa na maelezo ya mwanaume, atakuwa ametengeneza
mazingira ya kufanya mtoko uwe mzuri na usiyo chosha. Kuna baadhi ya
wanawake wao hukaa kimya tu na kusikiliza kama mwanaume ataongea nini na
hata kama mwanaume akiongea wao watakuw wanaitikia tu na hivyo kumfanya
mwanume asijue kama anachozungumza kinamvutia mwanamke huyo au
anamchopsha.....
12. Jipende mwenyewe: hakuna binadamu mkamilifu na wanaume huwa
hawatafuti mwanamke aliyekamilika, bali wanatafuna mwanamke
atakayewakubali na anayejipenda mwenyewe kwani kama mtu akijipenda
mwenyewe, ni dhahiri atawapenda wengine.
Mwanamke jipende mwenyewe..............
No comments:
Post a Comment