WADAU WAALIKWA KUSHIRIKI TAMASHA LA UTAMADUNI HANDENI DES.14

Posted in
No comments
Saturday, December 7, 2013 By danielmjema.blogspot.com


YAH: MWALIKO WA TAMASHA LA HANDENI 2013
Husika na kichwa cha habari hapo juu. Ukiwa kama mdau wa Handeni, mwananchi na mzalendo wa Tanzania, unaombwa kuhudhuria Tamasha la Utamaduni, maarufu kama ‘Handeni Kwetu 2013’, litakalofanyika katika Uwanja wa Azimio,  Jumamosi ya Desemba 14 mwaka huu.

Katika tamasha hilo, tutapata fursa ya kuangalia ngoma mbalimbali za utamaduni kutoka katika vijiji vya wilaya ya Handeni, kama vile Kweingoma, Kwamatukutu, Kwediamba, Kwachaga pamoja na vikundi vingine vya Handeni Mjini.

Tunapenda sana kushirikiana na wewe katika tamasha hili linaloanza kwa mara ya kwanza katika wilaya hii ya Handeni, mkoani Tanga. Kuanzishwa kwa tamasha hili ni sehemu ya kushirikiana kwa karibu na viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika Tamasha hili, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye pia ni Mbunge wa Handeni, Dkt Abdallah Kigoda. Tamasha hili litaanza na matembezi Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Handeni, saa 2:00 na kuelekea Uwanja wa Azimio, ambako huko litaisha saa 12 za jioni.

Kama mdau wetu wa maendeleo, tunakuomba tushirikiane kutangaza, kuthamini na kukuza utamaduni wetu ili iwe njia ya kuchangia maendeleo yetu. Hakuna kiingilio. Pia unaombwa kujigharamia mwenyewe katika ujio wako kwenye tamasha hili. Tunashukuru kwa ushirikiano wako na unakaribishwa sana katika Tamasha hili.
Wako katika Ujenzi wa Taifa.
Mratibu Mkuu
Kambi Mbwana
Wabsite: HANDENI KWETU, www.handenikwetu.blogspot.com
+255 712053949
+255 753806087
xxxxx

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .