WAGENI WANAENDELEA KUKIMBIA S.KUSINI
Posted in
No comments
Saturday, December 21, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Mataifa ya nje yanaendelea kuwaondosha raia wao Sudan Kusini baada ya ghasia za kikabila za juma zima.
Wakuu wanasema mawaziri kutoka nchi za jumuia ya IGAAD wanajaribu kuwasiliana na aliyekuwa makamo wa rais, Riek Machar, ili kujaribu kumaliza ghasia za kikabila zinazoendelea.Hapo jana ujumbe huo ulikutana na Rais Salva Kiir, ambaye alikariri kuwa anataka kufanya mazungumzo na mpinzani wake Riak Machar.
Rais Kiir hakutoa shuruti yoyote.
Bwana Machar hajulikani aliko na amewahi kusema kuwa yuko tayari tu kujadili kujiuzulu kwa rais.
Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Marekani, John Kerry, anamtuma mjumbe wake maalum, Donald Booth, kwenda Juba kujaribu kuhimiza mazungumzo.
Mashambulio kwenye mitambo ya mafuta katika jimbo la Unity, kando ya mpaka wa Sudan, yameleta wasi-wasi kuwa uchimbaji wa mafuta unaweza kusimama kabisa katika nchi ambayo pato lake kubwa linatokana na mafuta.Vyombo vya habari vinasema wafanyakazi zaidi ya 16 kwenye sekta ya mafuta wameuwawa na mamia wamekimbia.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :