Wednesday, February 12, 2014

BREAKING NEWZZZZZZZ: STOO YA CCP YAWAKA MOTO

TAARIFA zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa, Stoo ya kuhifadhia vifaa vya maaskari katika chuo cha mafunzo ya  polisi Moshi (MPA) maarufu kama CCP, imewaka moto.

Kwa mujibu wa taarifa hizo zilizothibitishwa na Mkuu wa Chuo hicho, CP-Matanga Mbushi, moto huo ulianza majira ya saa 3:45 alasiri.

Akizungumza na Kijiwe chetu Blog, Kamanda Matanga Mbushi amesema kuwa chanzo cha moto huo haujabainika japo moto huo unaonekana kuanzia katika Nguzo ya Umeme ulioko jirani na jengo la stoo.

Amesema maaskari wake walishirikiana kuuzima moto huo na kuokoa vifaa vingi na kwamba kinachoendelea kwa sasa ni zoezi la kufanya tathmini ambapo taarifa kamili zitatolewa baadae.


Kamanda huyo anatarajia kukutana na waandishi wa Habari Kesho asubuhi ambapo taarifa kamili ya chanzo na athari ya moto huo itatolewa.

No comments:

Post a Comment