Thursday, February 20, 2014

WANAWAKE WALIOBAKWA KUFUATIA MAPIGANO LIBYA KUFIDIWA

Wanawake wa Libya waliathiriwa zaidi na vita nchini humo
Waziri wa Sheria nchini Libya ,salaha al-Marghani,amesema kuwa Baraza la mawaziri limekubaliana kuwa Wanawake waliobakwa wakati wa harakati na maandamano ya kuuangusha utawala wa aliyekuwa Rais wa taifa hilo Muammar El Gaddafi mwaka 2011 watambuliwe kuwa waathirika wa vita.

Amesema makubaliano hayo yanayohitaji kuidhinishwa na Bunge kabla ya kuwa Sheria yatamfanya mwanamke awe sawa na wale wapiganaji waasi waliojeruhiwa halikadhalika watalipwa fidia.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu imekusanya ushahidi kuwa vikosi vya waliokuwa wakimuunga mkono Gaddafi walitekeleza vitendo vya ubakaji kama silaha.

Inaelezwa kuwa Wanawake wanaobakwa mara nyingi wamekuwa wakitengwa nchini Libya, hivyo haijafahamika wanawake wangapi watajitokeza.

No comments:

Post a Comment