BANUELIA BINGWA KIBO DIABETES AWARENESS
Posted in
Riadha
No comments
Monday, April 14, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Banuelia ameshinda mbio hizo upande wa wanawake akikimbia kwa dakika
31:18:53, nafasi ya pili ikaenda kwa mwanariadha chipukizi, Rose
Kasusura, mwenye umri wa miaka 14, kutoka katika klabu ya michezo ya
Kibo, ambaye alitumia dakika 45:13:52.
Nafasi ya tatu ya mtifuano huo ulioteka hisia za wengi ilikwenda kwa Teresia Kasim aliyetumia muda wa dakika 54:59:53.
Katika mbio za wanaume kilomita 8, mshindi alikuwa ni Marcel Ntandu
wa TPC, ambaye alitumia dakika 24:59:41, nafasi ya pili ikienda kwa
Matayo Milau wa Kili Athletic, aliyekimbia kwa dakika 25:01:37 na
nafasi ya tatu ikienda kwa Paulo Bajuta (dakika 25:32:80).
Akizungmza baada ya kushinda mbio hizo, Banuelia ambaye ni bingwa wa
taifa katika mbio za nyika, alisema kuwa ameamua kujipumzisha na
mashindano makubwa, lakini anatumia mashindano madogo madogo kama hayo
kujiweka sawa kabla ya kurudi upya katika mbio.
Alisema kwa muda mrefu amekuwa kimya, hivyo sio sahihi kurudi
uwanjani na anachokifanya hivi sasa ni kuhakikisha anarejea makali
yake, huku akiahidi kuwa hivi karibuni watu wamtarajie Banuelia
waliyekuwa wamemzoea.
Kwa upande wake, Meneja Msaidizi wa Benki ya Akiba (ACB), Tawi la
Moshi, Damari Kanyama, alisema lengo la kudhamini mbio hizo ni kutokana
na kutambua umuhimu wa michezo katika afya ya binadamu na kuongeza
kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza kama
kisukari.
Naye Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Benedeth Ollomi, alisema
wameamua kushiriki mbio hizo kama sehemu ya mpango wao wa afya kupitia
michezo na mazoezi na kuongeza kuwa KCMC imejipanga kuhakikisha
wanatumia michezo kuhamasisha kampeni dhidi ya kisukari ambayo imaenza
kushika kasi mkoani Kilimanjaro.
Mbio hizo zimeratibiwa na klabu ya michezo ya Kibo na kudhamniniwa na
KCMC, Japhary Dispensary, Zumba land, ACB, Central Palace, Honest
Block Reboring nk, ambapo washindi walikabidhiwa viatu vya kukimbilia
na vyeti.
SOURCE:Tanzania Daima
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :