Mb Dog akamilisha mbili mpya bomba balaa
Posted in
Muziki
No comments
Tuesday, June 24, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Msanii Mb Dog pichani.
Kukamilika kwa nyimbo hizo ni mwendelezo wa mikakati ya
msanii huyo kufanya kazi nzuri ili kumuweka katika kiwango cha juu katika
tasnia ya muziki wa kizazi kipya.
Akizungumza leo mchanaa jijini Dar es Salaam, Mb Dog alisema kwamba
nyimbo hizo amezirekodi katika Studio yake ya Macoppa, zilizopo jijini Dar es
Salaam.
Alisema kuwa nyimbo hizo zinaungana na ile ‘Mbona Umenuna’
aliyoachia mapema mwezi uliopita na kupokewa kwa shangwe na wadau wa Bongo
Fleva Tanzania.
“Hizi ni nyimbo mbili mpya na ambazo naamini zitapokewa kwa
shangwe na wadau mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini.
“Naamini kila kitu kitakwenda vizuri kuhakikisha kuwa mambo
yanakuwa mazuri, ukizingatia kuwa mipango iliyopo mbele yangu ni kufanya kazi
ya maana ili nionyeshe ukomavu wangu kisanaa,” alisema Mb Dog.
Mb Dog ni mmoja wa wasanii wanaotambulika kwa umahiri wao
katika tasnia ya Bongo Fleva, huku akikumbukwa kwa nyimbo zake, ukiwamo ule wa
Latifa na nyinginezo.
xxxxxx
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :