MTOTO WA MIAKA 9 AWEKA REKODI YA KUFIKA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO KWA KUPITIA NJIA NGUMI YA UMBWE
Posted in
Utalii
No comments
Sunday, July 6, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Idda katika safari yake |
Mwandishi wetu, Moshi
MSICHANA Idda Baitwa (9), ameweka rekodi ya kuwa mtanzania wa kwanza mwanamke kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro akiwa na umri mdogo zaidi kwa kutumia njia inadaiwa kuwa ngumu zaidi ya Umbwe -Kibosho.
Idda ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne, katika shule ya msingi mnazi, iliyoko manispaa ya Moshi, mkoani Kilimajaro, alifanikiwa kufika katika kilele cha mlima huo mrefu zaidi barani Afrika juzi majira ya saa 10:55 alfajiri.
Akizungumza na Kijiwe chetu Blog, majira ya saa 10:50 alasiri baada ya kufika katika geti la Mweka kushuka kutoka mlimani hapo, Idda aliwataka Watanzania kutembelea vivutio vya utalii kama njia ya kuwavutia wageni wengi nakuongeza pato la taifa kupitia utalii wa ndani.
"Nimefarijika sana kuingia katika kumbukumbu, ndoto yangu imetimia, Watanzania tuwe tayari kuthubutu, tujitokeze kutembelea vivutio vya ndani, moja kuongeza pato la Taifa, lakini pia kuwavutia wageni wengi
kupanfda mlima na kutembelea vivutio vingine," alisema Idda.
Alisema kuna haja kwa wazazi kuwahamasisha watoto wao kutembelea vivutio vya ndani kwani itasaidia kuwaongezea maarifa katika masomo yao hasa masomo ya uraia.
Idda alisema kwa muda mrefu amekuwa akitamani kuupanda mlima huo kama njia ya kuthibitisha uzalendo wake ambapo pia amesema atakuwa balozi wa kutangaza mlima huo kwa wanafunzi wenzake kwa lengo la
kuwahamassisha kuupanda na kujionea maajabu yake.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama cha waongoza watalii mlima Kilimanjaro (KGA), Respicious Baitwa, ambaye ni Baba mzazi wa mtoto huyo, alisema Safari yao ilikuwa nzuri na kwamba changamoto pekee ni
la misuli kufa ganzi yaliyomsumbua mtoto Idda.
Baitwa mwenye ndoto ya kupanda vilele saba akiwa tayari ameshapanda vilele vitano, aliitaka serikali kupitia wizara ya Maliasili na utalii kuangalia swala la malipo kwa waongoza watalii na wapagazi kwa lengo la kuwapa moyo zaidi wa kutangaza utalii wan chi hii.
"Tunamshukuru Mungu safari yetu imekwenda salama, tumefika kileleni na sasa namtambulisha kwenu Mtanzania wa kwanza kufika kilele cha mlima huu akiwa na umri mdogo zaidi,
tulichagua njia ya Umbwe kwa sababu ndio njia ngumu zaidi kati ya yote, kuna watu wenye umri mdogo, kutoka nje ya nchi ambao walifanikiwa kufika kilele ni lakini kwa kupitia njia nyingine rahisi ambazo hazina vikwazo vingi kama ilivyo umwe," alisema baitwa
Nao Lightness Sebastian na Leah Baitwa, ambao waliongozana na Mtoto huyo, walisema ili nchi iweze kupata mapato mengi ipo haja kwa serikali kuendelea kuwahamasisha wanafunzi kuzitembelea hifadhi hasa wanapokuwa likizo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :