Shirika la ndege la flydubai linasherehekea ukuaji wake wa haraka katika Afrika Mashariki na uzinduzi wa safari mbili za ndege za Tanzania

Posted in
No comments
Sunday, October 26, 2014 By danielmjema.blogspot.com


Njia hizo mpya zinasisitiza ukuaji wa haraka wa flydubai barani Afrika

DAR ES SALAAM, Tanzania, October 22, 2014/ -- Uzinduzi wa safari za ndege za Dar es Salaam na Unguja za shirika la ndege la flydubai (http://www.flydubai.com) lililo na makao yake Dubai ziliwasili nchini Tanzania leo. Njia hizo mpya zinasisitiza ukuaji wa haraka wa flydubai barani Afrika, na kukuza mtandao wa shirika hilo la ndege mara mbili likiwa na vituo 12 mwaka huu.

flydubai iliingia soko hili mnamo 2009 na safari za ndege za Jibuti, na mnamo 2011 Addis Ababa ikawa kituo cha pili cha flydubai katika Afrika Mashariki. Mnamo 2014, flydubai iliongeza njia sita mpya barani humu kwa kuanzisha safari za ndege za kuenda Burundi, Rwanda, Uganda na vituo vitatu nchini Tanzania.

Akizungumza kuhusu uanzishaji wa safari za Tanzania, Ghaith Al Ghaith, Afisa Mkuu MTendaji wa flydubai, alisema: "Umoja wa Falme za Kiarabu umetambua uwezo mkubwa katika masoko yanayokua ya Afrika Mashariki, kama vile Tanzania. Tunaendelea kufanya kwa bidii kusaidia malengo ya usafiri, biashara na utalii kwa kuimarisha muungano wa moja kwa moja katika ya Umoja wa Falme za Kiarabu na masoko haya ya Afrika."

Wawalikishi wa flydubai wakiongozwa na Sudhir Sreedharan, Naibu Mkuu wa Rais wa Biashra (GCC, Bara Dogo na Afrika), walilakiwa na tamasha za uzinduzi zilizofanyika katika viwanja vya ndege vya Dar es Salaam na Unguja mnamo 22 Oktoba 2014. Kati ya maofisa wakuu  waliozilaki ndege hizo za uzinduzi walikuwa Mheshimiwa Janet Z. Mbene (Mbunge), Naibu wa Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Dkt Omary Mjenga, Balozi Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu na Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu, Waziri wa Nchi.

"Kasi ya upanuzi wa safari za flydubai katika Afrika Mashaiki imeongezwa. Njia sita kati ya 23 mpya tulizozindua mwaka huu ziko barani Afrika. Uwezo tunaoona katika soko hili upeo mdogo wa uwezekano mkubwa kwani bado ni eneo ambalo halihudumiwi ipasavyo. Tuna furaha kuhusu safari zetu mpya za ndege nchini Tanzania, zitakazokuwa maarufu sana na abiria wetu ikiwa ni wa starehe au biashara," alisema Sreedharan.

Hivi karibuni Tanzania imeibuka kama mbia muhimu wa kibiashara wa Dubai na ni kati ya wabia wakubwa wa biashara zisizo za mafuta barani Afrika ikifikisha Dola bilioni 1.86 za Marekani mwaka jana katika jumla ya mapato ya biashara ya mwaka, hii ni kulingana na bata mypa kutoka Chama cha Wafanyabiashara cha Dubai.

flydubai ilianza kutumia ndege zake mpya za Boeing 737-800 zilizo na Kitengo cha Biashara katika safari zake za Dar es Salaam, Kilimanjaro na Unguja kuanzia tarehe 16 Oktoba, 2014, ikiwapa abiria kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu huduma rahisi sana, ya kiwango cha juu na ya kuaminika iliyo na chaguo ya kuunganisha safari kuelekea kitovu cha safari za anga Dubai.

Zaidi ya safari zake tatu nchini Tanzania, flydubai imeunda mtandao mpana barani Afrika na safari za ndege za Addis Ababa nchini Uhabeshi, Alexandria nchini Misri, Khartoum na Port Sudan nchini Sudani, mji mkuu wa Jibuti, Juba nchini Sudani Kusini pamoja na Bujumbura nchini Burundi, Entebbe nchini Uganda na Kigali nchini Rwanda.

Maelezo ya Safari za Ndege:

Dar es Salaam
flydubai itakuwa na safari za ndege za kila siku kati ya Dar es Salaam na Dubai kuanzia tarehe 16 Oktoba 2014.
FZ670 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 6:20 machana saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:55 jioni saa za ndani.
FZ672/674 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 12:20 jioni saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 7:00 usiku saa za ndani.
FZ669/671/673 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:40 asubuhi saa za ndani, iwasili Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 5:20 asubuhi saa za ndani.

Nauli za safari ya pande mbili
Nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Dar es Salaam hadi Dubai itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa, huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 1,499 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa. Hizi ni nauli spesheli za uzinduzi zitakazotumika kwa mwezi mmoja.

Kilimanjaro kupitia Dar Es Salaam
flydubai itakuwa na safari mbili za ndege kwa wiki kati ya Kilimanjaro na Dubai kupitia Dar Es Salaam kuanzia tarehe 17 Oktoba 2014.


Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .