TANZIA: MWANDISHI WA HABARI WA MTANZANIA AMEFARIKI DUNIA GHAFLA

Posted in
No comments
Wednesday, November 19, 2014 By danielmjema.blogspot.com


Innocent Munyuku enzi za uhai wake.Mwandishi nguli anayeandikia gazeti la MTANZANIA, linalochapishwa na Kampuni ya New Habari (2006) Ltd. yenye maskani yake Sinza Kijiweni Jijijini Dar es salaam, INNOCENT MUNYUKU, amefariki dunia ghafla nyumbani kwake Rombo Kimara three hrs back. Taratibu zingine nitawajulisha.

HAFIDH KIDO ANASEMA...


What is going on here?....someone called me but am not yet to believe this..



KAMBI MBWANA ANASEMA HIVI...


Namjua Sana Kaka Innocent Munyuku. Alikuwa Mmoja Wa Watu Walionijenga Katika Tasnia Ya Habari. Kupokea Kwa Taarifa Ya Kifo Chako Kilichotokea Usiku Wa Kuamkia Leo Nimeshtushwa Sana. Pumzika Kwa Amani Kamanda Munyuku. Umetuacha Wapweke Komrade. Mimi Na Wadau Wote Wa Taasisi Ya Handeni Kwetu Foundation Tumepokea Taarifa Hizi Kwa Masikitiko Makubwa, Hapa Handeni, Mkoani Tanga. Poleni Sana New Habari 2006 Ltd, Poleni Sana Waandishi Wote Duniani.

MWANI DE OMAR NYANGASA NAE...
Ni vigumu kuamini, naona shida kuzungumzia kwa kua ni kitu ambacho sikiamini, eti leo kaka zangu Innocent Munyuku na Baraka Karashani hatunao, wamekufa siku moja, juzi nilipata taarifa za kuumwa Baraka, jana nikaenda hospitali na dada yangu Grace Hoka kumuangalia tulitokwa na machozi Baraja hakua na hali nzuri tukajipa moyo atapona na tukamfariji mkewe kua asife moyo Baraka atakua na nguvu nikaondoka, Leo asbh naamshwa na simu eti Innocent amefariki nilipigwa na butwaa nikatoka hadi kwake ukweli nilishuhudia mwili wake ukiwa kitandani umefunikwa nikajiridhisha tukaambatana na wafanyakazi wenzangu hadi Lugalo kuuhifadhi mwili nikiwa njiani nikiwaeleza habari za Baraka wote wakasema twendeni tukamuone, ghafla nilibadili mawazo nikasema baada ya kumhifadhi Innocent sitaenda wodini anaetaka aende, kumbe nilikua nakataa kushuhudia umauti wake Baraka, hadi kufikia hapa nilipo watu hawa wamechangia kwa kiasi kikubwa mimi leo kuwa Mwani De Omar Nyangassa kimawazo, ushauri na hata kunipa ujasiri nilionao, ni siku ngumu sana kwangu, naumia, nalia kwa uchungu ila mwisho namuomba Mwenyez Mungubaziweke roho zenu mahala pema peponi,

OLIPA ASSA

ulikuwa mcheshi kaka nitakukumbuka daima, umetangulia tu

HAPPINESS KATABAZI

NOVEMBA 19 Mwaka 2014 saa 5:11 asubuhi ya leo, nikiwa ofisini Kwangu katika Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), Mikocheni Dar Es Salaam, nikiifungua page yangu ya Facebook ndiyo nikakutana na taarifa ya Tanzia ya kifo Cha Mwanahabari ,Innocent Mnyuku ambayo imewekwa kwenye ukurasa wa mwanadishi wa Habari, Albert Kawogo.

JOSEPH SHALUWA

NAKUMBUKA vizuri sana. Ilikuwa asubuhi ya saa 4, niliamua kudamkia Ofisi za Uhuru Publication ili kuonana na Charles Mateso (akiwa mhariri wa Burudani) lakini nikaonana na wewe kaka Innocent Munyuku kuhusu makala zangu kuanza kutoka katika Gazeti la Burudani. Uliponiona ulitabasamu, ukaniambia: 'Dogo makala zako nzuri. Nimejadiliana na Mateso (Charles), tumekupa safu ya Simulizi za Mapenzi. 

Endelea kuandika mdogo wangu.' Wewe na Mateso mlinipokea vizuri sana na kunipa moyo. Hiyo ilikuwa mwishoni mwa 2004. Leo hii siamini kama umeondoka kaka. Namuomba Mungu akusamehe dhambi zako na kukuweka pema. Pole kwa familia ya Munyuku, poleni sana New Habari 2006. RIP kaka Munyuku.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .