Iringa kuongeza vivutio vya Utalii
Posted in
Utalii
No comments
Monday, December 22, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, amesema mkoa wake utapata jengo la makumbusho la kisasa kabisa litakalokuza sekta ya utalii pamoja na kuwawezesha wajasiriamali wadogo na kuongeza ajira kwa jamii ya Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza.
Mkuu huyo wa mkoa amesema Nyanda za Juu kusini licha ya kuwa na vivutio vingi vya utalii, hata hivyo bado rasilimali hiyo haijatumika ipasavyo ili kuweza kuchangia katika kukuza maisha ya jamii hii kutokana na kukosekana kwa ufahamu bora miongoni mwa wanajamii juu ya umuhimu wa wa urithi huu wa utamaduni na utalii kwa maendeleo ya sekta ya utalii na biashara.
Masenza amesema jengo hili la kisasa la makumbusho litakuwa katika iliyokuwa ikifahamina kama Iringa Boma, ambapo sasa litatumika kwa ajili ya kuonesha mambo ya urithi wa kihistoria na kuvutia watalii duniani kote kuja kutembelea Tanzania hasa mkoa wa Iringa.
Mkuu huyo wa mkoa amesema ajira nyingi zitaongezeka kuanzia ukarabari wa jengo hilo la zamani na vilevile wasomi wa taaluma ya makumbusho na uhifadhi wataajiriwa katika kuhudumia makumbusho haya ya kisasa.
CHANZO: EATV
Habari Zingine
- SAFARI YA MABALOZI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KATIKA SIKU YA KWANZA
- Iringa kuongeza vivutio vya Utalii
- NYALANDU ASISITIZA SERIKALI HAINA MPANGO WA KUWAONDOA WAMASAI LOLIONDO
- MANDHARI MWANANA YAWAVUTIA WATALII WA NDANI HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO
- SIKU YA PILI ILIVYOKUWA KWA MABALOZI WAKATI WAKIPANDA MLIMA KILIMANJARO.
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :