18 KUPATIKANA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015 MCHUJO WAANZA RASMI JIJINI DAR
Posted in
Habari na Jicho Pevu la Kijiwe
No comments
Tuesday, June 2, 2015
By
danielmjema.blogspot.com
Muwakilishi
wa Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa TBS Joseph Masikitiko katika
Hafla ya maamuzi ya fomu za shindano la mamashujaa wa Chakula Bi. Stella
E. Mrosso wa kwanza kushoto, wa pili kutoka kushoto ni Tusfaye Legesse Obole President's Delivery Bureau, Manager Agriculture Productivity na Mratibu wa Programu kutoka Care International in Tanzania Maureen Kwilasa ambaye ni Mkuu wa mahabara ya Chakula TBS akifungua rasmi
hafla hiyo ya kuanza kuzihakiki fomu hizo .
Eluka
Kibona, Meneja
Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea juu ya shindano la Mama shujaa
wa Chakula .
Mratibu wa Programu kutoka Care International in Tanzania Maureen Kwilasa akisisitiza jambo wakati wa Hafla hiyo
Mkurugenzi
Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiwashukuru TBS , Majaji pamoja na
washiriki ambao ndio watazipitia fomu hizo kabla hazijafika kwa majaji.
Mkuu wa maabara chakula TBS Stella E. Mrosso aliye Mwakilisha Mgeni rasmi katika hafla hiyo akimkabidhi rasmi fomu za shindano la mama shujaa wa chakula Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster kwa ajili ya kuanza kufanya maamuzi.
Vijana
wenye fani mbalimbali kutoka vyuo vikuu na taasisi mbalimbali wakiwa
katika mchakato kwa kuzipitia Fomu zote za maombi ya kushiriki shindano
la mama shujaa wa Chakula 2015
Hafla ikiwa inaendelea
****
Shindano
la mama shujaa wa chakula limeingia katika hatua mpya baada ya zoezi la
kukusanya fomu za washiriki kutoka mikoa mbalimbali nchini kupitiwa na
majaji kwa ajili ya mchujo ambapo washiriki 18 watapatikana kisha
baadaye 15 bora ambao wataingia kijijini kwa ajili ya mchakato wa
kugombea nafasi ya mama shujaa wa chakula mwaka 2015.
zoezi
la kusahihishwa fomu limezinduliwa mapema leo hii na mwakilishi wa
Mkurugenzi Mtendaji wa TBS, Joseph Masikitiko ambaye ni Mkuu wa Maabara
na Chakula TBS, Bi. Stella Mrosso akiwa sambamba na Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Oxfam Tanzania, Jenny Foster na majaji watakaopitia zoezi
zima la mchujo wa fomu hizo.
Akizungumza
na wageni waandishi wa habari katika uzinduzi huo Mkuu wa Maabara na
Chakula, Bi. Stella Mrosso alilisifu shirika la Oxfam kuwa mstari wa
mbele katika kupigania haki za wanawake, umiliki wa ardhi na kuhamasisha
uzalishaji wa chakula kwa wazalishaji wadogo wadogo.
Bi.
Stella alisisitiza kuwa kila mzalishaji anapaswa kuzalisha bidhaa bora
ili kushindana na soko la ndani na la nje huku akifafanua kuwa kwa
kupitia SIDO, TFDA na Wizara ya Afya, wazalishaji wadogowadogo watakuwa
na uwezo wa kupata kibali kutoka TBS bure na kuongeza kuwa wakina mama
nchini watumie shindano la mama shujaa wa Chakula kama chachu ya
kujitokeza kwa wingi katika mashindano yanayofuata huku wengine
wakijifunza uzalishaji bora kupitia mashindano hayo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :